Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

SERA MBOVU ZA UCHUMI SI RAFIKI WA WALALAHOI: PROF. LIPUMBA

$
0
0
TAIFA letu limekuwa lilikabiliwa na mdororo mkubwa wa uchumi uliosababishwa na sera ambazo si rafiki kwa walalahoi. Suala la kuanzisha vijiji vya ujamaa kuliwaondolea motisha wakulima na kuona kama kuna ukiritimba kwani aliyekuwa akifanya kazi kwa bidii aliwekewa vikwazo.

Katika mkutano wa Taasisi ya utafifiti katika masuala ya kiuchumi na kupunguza umasikini (REPOA) uliofanyika Machi 28, mwaka huu Jijini Dar es Salaam, Profesa Ibrahim Lipumba aliainisha baadhi ya masuala muhimu ya uchumi huku akiishauri Serikali hatua za kuchukua.

Profesa Lipumba, ambaye ni bingwa wa uchumi duniani, anasema wakati wa ujamaa wafanyabiashara wengi waliokuwa katika sekta binafsi walikuwa wanajua namna ya kuitumia serikali na sekta ya umma kuweza kupata masilahi ambapo kutokana na hali hiyo ndipo rushwa ikaanza kwenye ukiritimba wa dola ndani ya uchumi.

Anasema, hadi kufikia mwaka 1985 Tanzania ilikuwa na hali mbaya zaidi kutokana na madeni yaliyoshindwa kulipwa na Serikali hata kufikia Mashirika ya umma kupata hasara na hayakuweza kuendeleza ajira wala uzalishaji.

Anasema, wakati tukiingia katika urekebishaji wa uchumi huku tukiwa hatuna dira thabiti kwa wale wanaouziwa mashirika, tulishindwa kujua waliouziwa kama wanaweza kufanya kazi kama mikataba inavyosema.

Akitolea mfano, Profesa Lipumba anasema, wakati wakulima wa korosho wanaambiwa wasimuuzie yeyote zao hilo zaidi ya chama cha ushirika, bado chama hicho kinawakopa na kusababisha kupungua kwa motisha kwa mkulima.

“Miundombinu yetu ni mibovu kwani huwezi kuwa na uchumi wa kisasa bila ya kuwa na umeme wa uhakika, uwekezaji wetu katika umeme umekuwa mdogo”

“Ni wazi uwekezaji mwingi ulikuwa ukitegemea misaada kutoka nje, lakini pamoja na misaada hiyo, bado tumeshindwa kukusanya mapato na kuendeleza uwekezaji nchini” anasema Profesa Lipumba.

Mtaalamu huyo wa uchumi, anasema anasema madini yamekuwa ni sababu kubwa kwa serikali kutegemea misaada ya wahisani katika kupanga bajeti yake, kwani imekuwa haikusanyi mapato katika sekta ya madini.

“Wawekezaji wamefanikiwa kututeka kwani kampuni zote kubwa za wanasheria wetu maarufu ndio wanakuwa wanasheria wa Kampuni za migodi, na Watanzania wengi maarufu wamepewa nafasi ya kuwa wenyeviti wa bodi au wajumbe wa bodi.

“Kampuni zimekuwa bingwa wa kuchukua watu wakubwa kuwa na vyeo vya juu, hivyo inahitaji kiongozi wa nchi uwe na nguvu ya umma au jasiri kuhakikisha nchi nayo inapata fedha za kutosha.

“Tanzania tumegundua kuwepo kwa gesi maeneo ya Mkuranga, Mtwara na Kilwa lakini tusipokuwa makini kwa kuangalia mikataba bado haitawanufaisha Watanzania.

“Tunatakiwa katika madini tupate angalau mapato ya asilimia 30 yaingie katika pato la serikali ili tuyaingize yasaidie katika sekta za afya, miundombinu, elimu na kilimo,” anasema Profesa Lipumba

Anasema tofauti na hilo, inabidi kujifunza kwa wengine huku akitolea mfano Botswana kwa kueleza kwamba katika madini yao ambayo mengi ni almasi inayofikia asilimia 70, inatumiwa kwa kuwanufaisha wananchi moja kwa moja au kuingia katika mapato ya serikali au mapato ya umma.

Profesa Lipumba anasema nchi inapaswa kuwa na mikataba ya aina hiyo ambayo ina tija kwa wananchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>