↧
KIJIWE CHA UGHAIBUNI
↧
RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI, KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
PICHA NA IKULU
↧
↧
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI"
1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.
2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.
3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani? (P.T)
4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?
6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
↧
LIPUMBA, WAFUASI 32 WA CUF WATIWA NDANI JIJINI DAR
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiwapungia mkono wafuasi wake mara baada ya Polisi kuyasambaratisha maandamano ya amani ya chama hicho yaliyokuwa na lengo la kuwakumbuka wanachama wenzao, walioteswa na kuuawa kwa kipigo cha Polisi huko Zanzibar Januari 27 mwaka 2001.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba (katikati) akiwa amewekewa ulinzi na wafuasi wa chama hicho wakati Polisi walipozuia maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike leo kuanzia Temeke Hospitali hadi Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam. (Na
Mpiga Picha Wetu)
Haki......
Walinzi maalum wa CUF wakiwa wameimarisha ulinzi katika gari alilopanda Mwenyekiti wa chama hicho.
Polisi wakizuia maandamano ya CUF katika eneo la Mtoni.
Mlinzi wa Prof. Ibrahim Lipumba akizozana na askari wa kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakati walipota kumkamata bosi wake.
Prof. Lipumba akiwa katika gari la Polisi
Mfuasi wa CUF akiwa chini ya ulinzi.
Prof. Lipumba akizungumza na maofuisa wa Polisi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.
Awali polisi ilizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.
Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.
“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.
Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.
Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.
“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.
Alisem sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.
↧
RAIS BARACK OBAMA AENDA SAUDI ARABIA KUHANI MSABA WA MFALME ABDULLAH
Rais Barack Obama ameongoza ujumbe mkubwa wa Marekani, nchini Saudi Arabia kufuatia kifo cha mfalme Abdullah.
Rais Obama alikatiza ziara yake ya nchini India ili kupata fursa ya kuhani msiba wa mfalme huyo, ambapo pia alikutana na mfalme mpya wa nchi hiyo Salman.
Rais Obama aliambatana na maafisa maarufu wa chama cha Republican wakiwemo waliyowahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James Baker na Condoleezza Rice.
↧
↧
KIOTA CHA OLYMPIA PUB CHAUNGUA MOTO JIJINI DAR
Kiota cha maraha kiitwacho Olympia kilichopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam chaungua moto leo jijini Dar es Salaam ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema..
Moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto.
Zima moto hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako saa 12 asubuhi wakiwa na maji kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.
Lango la kuingilia Club.
Muonekano wa sasa baada ya kuungua.
↧
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akicheza ngoma ya asili ya Mkoa wa Kagera wakati alipokuwa akilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella .
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella akimkabidhi Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing Hati na ramani eneo lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichoahidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana.
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akipokea zawadi ya ramani ya Afrika Mashari iliyochorwa kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto.
Balozi LU akisaini kitabu cha wageni Bukoba airport.
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akitoa zawadi kwa wanafunzi.
Picha ya Pamoja.
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili kukagua eneo lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichohaidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana Oktoba 2014.
Akimkaribisha mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa John Mongella alimweleza Balozi LU kuwa mkoa wa Kagera una fursa nyingi za uwekezaji ambazo ni pamoja na uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo vya kusindika bidhaa mbalimbali ili kuinua uchumi wa wananchi na mkoa kwa ujumla.
Bw. Mongella alimwomba Balozi LU kufikiria kuleta wataalamu wa afya hasa madaktari kutoka nchini mwake hususani katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ili kutoa huduma kwani mkoa upo mbali sana na hospitali za Rufaa za taifa jambo ambalo huleta usumbufu kwa wagojwa wanaohitaji huduma za hospitali za rufaa.
Balozi LU katika kutoa salaamu zake alisema kuwa amefurahi kufika mkoani Kagera kwa mara ya pili na akasifu mkoa kwa kuwa na hali nzuri ya hewa na kubarikiwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Aidha, alisema kutokana na urafiki wa nchi mbili za Tanzania na China amefurahi kuwa sasa kutakuwa na alama ya urafiki huo katika mkoa wa Kagera.
Pamoja na kuusifia Mkoa wa Kagera imeisifia serikali ya Tanzania kwa kutekeleza miradi ya maendeleo,alisema kuwa ukipita mikoani unaona mabadiliko makubwa kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Ambapo alisema kuwa serikali ya China imewekeza na kutekeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya bilioni 3.15 dolla za kimarekani kwa mwaka 2013/2014.
Balozi LU alitembelea kiwanja cha hekta 26,000 kilichopo eneo la Kahororo katika Halamashauri ya Manispaa ya Bukoba ambapo chuo cha ufundi (VETA) kitajengwa na kujionea mwenyewe kitakapojengwa chuo hicho. Pia alitembelea shule ya Mgeza Mseto ambako aliwahi kutembelea na kutoa msaada wa komputa ili kuona wanafunzi wa shule hiyo maendeleo yao.
Katika shule ya msingi Mgeza Mseto yenye wanafunzi wa bweni na kutwa pia inapokea watoto wa aina tatu, watoto wenye albinisimu, watoto wenye ulemavu wa viungo, na watoto wa kawaida, Balozi LU alisema amefurahi kuwaona tena na kuhaidi kutoa msaada zaidi wa komputa ili watoto waweze kila mmoja kujifunza komputa.
Katika maelezo yake Balozi LU aliufananisha mkoa wa Kagera na Jimbo la Chandog la nchini China na kusema kuwa atahakikisha unaungaisha urafiki kati ya mkoa wa Kagera na jimbo hilo ili kuleta maendeleo zaidi Kagera. Vilevile alisema atahakikisha anfanya mpango wa Tanzania hasa mkoa wa Kagera unakuwa na utaratibu wa kubadilishana walimu kutoka nchini China.
Maeneo ya uwekezaji ambayo mkoa umeyatenga kwa ajili ya uwekezaji ni pamoja na Kilimo cha kisasa katika maeneo mbalimbali, Ufugaji wa kisasa wa samaki, Ujenzi wa bandari ya Kemondo(contena terminal) na ufugaji wa kisasa wa nyuki pamoja na ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA).
↧
RAIS KIKWETE AHAMASISHA MCHANGO WA DOLA BILIONI 7.5 KWA AJILI YA CHANJO YA WATOTO KWA NCHI MASIKINI DUNIANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Erna Solbergna Mwenkekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, wakiwa jijini Berlin, Ujerumani, wakati wa chakula cha mchana cha mazungumzo baada ya kumalizika kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, baada ya kumalizika kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti Mwenza wa Bill & Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates wakati wa chakula cha mchana cha mazungumzo na kuhusu kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo ya GAVI toka kwa mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo Bw. Dagfinn Høybråten kutokana na mchango wakd mkubwa katika kuundwa na hatimaye kusimia utekelezaji wa mipango ya GAVI hata kufanikisha upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kupokea tuzo ya GAVI toka kwa mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo Bw. Dagfinn Høybråten kutokana na mchango wakd mkubwa katika kuundwa na hatimaye kusimia utekelezaji wa mipango ya GAVI hata kufanikisha upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi
ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya
kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,
Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu wa Norway Mhe.
Erna Solbergna Mwenyekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates
Foundation, Bw. Bill Gates, wakiwa jijini Berlin, Ujerumani, kabla ya
kuanza kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa
kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global
Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa
ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500
wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba
wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, huku Waziri wa
Maendeleo ya Uchumi wa Ujerumani Bw. Gerd Muller, Rais wa Mali Mhe.
Ibrahim Boubacar Keïta jijini Berlin, Ujerumani, wakati wa chakula cha
jioni cha mazungumzo na harambee ya kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi
ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya
kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.PICHA NA IKULU.
↧
MGOMO WA WAFANYABIASHARA IRINGA BAADHI WAGOMA KUSHIRIKIANA
Askari wa FFU wakizunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa jana kama njia ya kulinda amani kwa wafanyabiashara ambao waliendelea kutoa huduma baada ya wenzao kuwa katika mgomo. |
MOja kati ya maduka mjini Iringa yakiendelea kutoa huduma mbali ya wafanyabiashara wengine kuwepo katika mgomo kushinikiza kuachiwa huru kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara Taifa Bw Johnson Minja. |
Maduka mtaa wa uhindini mjini Iringa yakiwa yamefungwa jana kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara nchini. |
Wananchi mbalimbali wa mji wa Iringa wakiwa katika soko kuu la mjini Iringa kupata huduma zao wakati sehemu mbali mbali huduma zikiwa zimesitishwa kufuatia mgomo wa wafanyabiashara nchini. |
Na matukiodaimaBlog.
BAADHI ya wafanyabiashara mkoani Iringa jana wamegoma kuungana na
wafanyabiashara wenzao nchini kushiriki mgomo wa kushinikiza jeshi la polisi kumwachia huru mwenyekiti wao wa chama cha wafanyabiashara nchini Bw Johnson Minja anayedaiwa kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
Wafanyabiashara hao waliosusia mgomo huo walifikia uamuzi huo kama hatua ya
kupinga uamuzi wa wenzao ambao walifunga maduka yao kwa siku nzima kuungana na wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam ambao walifanya hivyo .
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa na maeneo ya nje ya mji wa Iringa ulionyesha kuwa mgomo huo kukosa ushirikiano kutokana na baadhi ya maduka ya pembezoni mwa mji wa Iringa na yale ya vijijini na baadhi ya maduka ya katikati ya mji wa Iringa kuendelea na huduma kama kawaida huku wakiomba ulinzi kwa jeshi la polisi ili wao kuendelea kutoa huduma kama kawaida.
Huku cha kushangaza hata baadhi ya salun na bucha za nyama katika baadhi ya maeneo mjini hapa zilifungwa huku baadhi ya maduka yanazozunguka soko kuu la Iringa pia yakifungwa japo katika soko hilo umati mkubwa wa wananchi waliendelea kupata huduma kama kawaida .
Mmoja kati ya wafanyabiashara wa mji wa Iringa Bw JOhn sanga alisema kuwa ameshindwa kuungana na wafanyabiashara wa mji wa Iringa katika mgomo huo kutokana na shinikizo kubwa ambalo lilikuwa likionyeshwa na watu waliokuwa wakisambaza jumbe za mgomo huo juzi na jana kupitia kikundi cha watu kama 11 ambao wengi wao walikuwa wakitoa vitisho wakati wa kusambaza taarifa hizo.
"Kweli nimeshindwa kufunga duka langu leo kutokana na vitisho vya watu hao ambao wanatulazimisha kufunga kwa nguvu huku wakitambua kuwa si kila mfanyabiashara ni mwanachama wa chama chao hicho cha wafanyabiashara ....kutulazimisha kufunga biashara zetu ni kutunyanyasa sisi tusio wanachama na tambua kila mmoja ana maisha yake wao badala ya kukutana viongozi kwa ajili ya kulimaliza suala hilo wanataka wote tufunge maduka huu ni ushauri mbaya kuliko"
Hata hivyo alisema hajaweza kufunga na ataendelea kutoa huduma wakati wote wa mgomo wa wafanyabiashara hao kwani si lazima kila mfanyabiashara kuungana nao katika chama chao na kiongozi wao.
Huku mfanyabiashara Geofrey kalinga akieleza kusikitishwa na serikali kushindwa kuchukua hatua kali kwa kikundi hicho cha wafanyabiashara wachache ambao wanachochea mgomo huo na kuwakosesha wengine amani ya kufungua biashara zao na kuwa kuendelea kuchelewa kuchukua hatua ni kubariki migomo kama hiyo kuendelea.
Kwani alisema ni jambo la kushangaza kuona watu hao wachache wakitumia nguvu kuwazuia wengine kuungana nao katika mgomo huo huku wakitambua kuwa chama hicho ni chama cha hiari kujiunga ama kutojiunga hivyo walipaswa kushughulika na wanachama wao na sio wafanyabiashara wote.
"Haya ni mambo ya ajabu sana hivi inawezekana vipi hiki kikundi cha wachache kutulazimisha wafanyabiashara wote kujiunga na chama chao... sasa leo wanatutaka kufunga biashara kwa muda usiojulikana kesho watakuja na jambo jingine lakini swali la msingi hapa hicho chama chao kinatusaidia nini sisi ambao si wanachama tunapofungiwa biashara zetu ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kuchelewa kulipa kodi....ama wanatusaidia vipi na kodi kubwa ya mapango ya
vyumba vya biashara ambazo tumekuwa tukilipa .....kama jibu hakuna
basi watuache na wao waendelee na migomo yao"
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wafanyabiashara waliofunga maduka yao walisema kuwa sababu ya kufunga maduka kwa muda usiofahamika ni kutoka jeshi la polisi kumwachia huru kiongozi wao kitaifa Bw Minja anayedaiwa kukamatwa toka juzi na jeshi la polisi na hajulikani alipo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Iringa Suzana Ndelwa alisema kuwa kufungwa kwa maduka katika mji wa Iringa kumewaathiri wananchi kiuchumi kutokana na baadhi yao kutoka nje ya mji wa Iringa kufuata huduma za jumla ila kufungwa kwa maduka hayo kumeyumbisha uchimi wao na wa Taifa kwa ujumla na kuwa ilipaswa kwa upande wa mkoa wa Iringa mkuu wa mkoa huo kuingilia kati suala hilo.
Mbali ya baadhi yao kutoma kufunga maduka yao bado ule usemi wa kufa kufaana ulionekana kutawala katika maeneo mengi ya mji wa Iringa kutokana na mgomo huo baada ya baadhi ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga kunufaika zaidi na mgomo huo kwa kupanga bidhaa zao nje ya maduka yanayofanya biashara kama zao na kupata wateja zaidi kupitia mgomo huo huku baadhi ya wafanyabiashara wakionekana kuuzia bidhaa zao stoo na wengine kufungua maduka yao nusu mlingoti na kuendelea kutoa huduma kama kawaida.
Wakati wafanyabiashara hao wakiwa katika mgomo huo mjini Iringa, Mafinga
na baadhi ya wachache wa Ilula bado jeshi la polisi lilionekana
kuweka ulinzi wa kutosha katika maeneo ya wafanyabiashara hao
huku askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)) wakionekana
kuzunguka kila kona ya mji wa Iringa ili kuthibiti vurugu iwapo
zingejitokeza.
Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ama kamanda wa
polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ili kuweza kuzungumzia
jinsi mkoa ulivyojipanga kumaliza tatizo hilo la mgomo ama jeshi la
polisi lilivyojipanga kuwalinda wafanyabiashara ambao waligoma
kuungana na wenzao katika mgomo huo hazikuzaa matunda baada ya simu
za viongozi hao wawili kuita bila kupokelewa .
↧
↧
JANUARY MAKAMBA NA NDOTO YA VITUO VYA MICHEZO VYA KANDA
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi karibuni pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa January Makamba(Pichani juu) hivi karibuni ameainisha adhma yake ya kuinua kiwango cha michezo nchini.
Azma hizo zimo katika katika mazungumzo yake na Padre Privatus Karugendo ambayo yamechapishwa katika kitabu ambacho gazeti hili imekipata nakala yake ambapo ameainisha azma ya kujenga vitua vya michezo vya kanda vyenye hadhi
ya kiolimpiki.
Kwenye kitabu hicho, Makamba amejibu swali kwamba kitu gani kifanyike ili Watanzania waweze kujivunia wanamichezo wao. Makamba alisema, “Inafedhehesha sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho tumeshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika.
Mwaka huo huo wa 1980 ndio mara ya kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda medali za Olimpiki. Rafiki yangu Mzee Suleiman Nyambui na Mzee wetu Filbert Bayi ndio walitutoa kimasomaso kipindi kile. Ni muhimu kurekebisha hili.”
Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu katika medani ya kimataifa huku tasnia ya michezo ikiendelea kugubikwa na migogoro isiyokwisha. Kutokana na migogoro hii, Tanzania inaendelea kupoteza matumaini ya kung’aa katika medani za kimataifa.
Katika mazungumzo hayo na Padre Karugendo, Makamba alinukuliwa akisema, “Lazima tutambue kwamba maendeleo ya michezo yanatokana na vitu muhimu vitatu. Kwanza, ni lazima kuwepo na vipaji, bahati nzuri nchi yetu ina vipaji vya kutosha katika aina zote za michezo. Pili, ni miundombinu na mfumo wa kubaini na kuviendeleza vipaji hivyo, hii bado ni changamoto . Tatu, ni utawala, uongozi, na uendeshaji wa tasnia ya michezo, hii pia ni changamoto. Hivi vitu vitatu ni lazima viwepo ili tuweze kupata mafanikio kwenye medani ya michezo.”
Kama mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makamba anaungwa mkono na vijana wengi kutokana na kuendesha siasa zake kisasa, kibunifu na kuepuka malumbano ya jukwaani.
Katika mazungumzo hayo Makamba alielezea fikra zake alizonazo hasa hasa kwenye kuendeleza vipaji vya Watanzania ambapo alisema, “Ni lazima tuanzishe vituo vikubwa vya michezo au ‘sports academies’ kwenye kila kanda ya nchi yetu vyenye hadhi ya Kiolimpiki.”
Makamba aliongeza kwamba, “Kutakuwa na vituo sita vya aina hii katika nchi yetu ambavyo vitazungukwa na shule za msingi na sekondari za ‘boarding’. Vituo hivi vitakuwa na lengo la kukusanya wanafunzi wote kwenye kanda husika ambao wameonekana kuonyesha vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa. Ukweli ni kwamba bila kuendeleza vipaji katika mazingira mazuri, basi tusahau kabisa kufanya vizuri kwenye michezo. Hili linaweza kufanywa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi”.
Mheshimiwa January Makamba anakuwa mgombea wa kwanza wa Urais kuweka bayana mipango yake ya Tanzania Mpya katika maandishi. Anaendelea kufunguka kwamba katika tasnia ya michezo ni muhimu sana kuwekeza katika watoto. Zaidi ya hapo, kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na akademi na TFF iendeshe ligi kuu ya timu za watoto.
“Tufikie wakati ambapo timu za taifa za miaka 10 ijayo ziwe zinaandaliwa kuanzia sasa, na serikali itenge bajeti kila mwaka kwa timu hizo ili kuziwezesha kukaa kambini, kufanya mechi za majaribio na kuziwezesha kushiriki kikamilifu katika mashindano ya kimataifa. Mimi sio muumini wa hizi kamati za zimamoto kusaidia timu ishinde ghafla ghafla wakati siku zote watu hawafanyi maandalizi ya muda mrefu” alimalizia Makamba.
Makamba pia aligusia kuhusu suala la ukata na ufinyu wa bajeti unaokabili tasnia za michezo. Siku zote tunaona timu za taifa za olimpiki au jumuiya ya madola kukosa fedha za kukaa kambini ambapo huchangia katika matokeo hafifu.
“Huko nyuma, taasisi na mashirika ya umma yalikuwa na timu za michezo zilizokuwa zinafanya vizuri na kutoa michango kwenye maendeleo ya michezo. Kwa mfano, Pamba ya Mwanza, Sigara, Reli ya Morogoro, ushiriki huu ulichangamsha sana michezo na ni lazima turudishe utamaduni huu,” alimalizia Makamba.
↧
WANAKIJIJI KILOMBERO KUMBURUZA MAHAKAMANI MWEKEZAJI
Mkazi wa Kijiji cha Chiwachiwa kilichopo Tarafa Mgeta Kata ya Mbingu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Merkizedek Mazani (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mgogoro wa ardhi dhidi mwekezaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya Union ambaye anadaiwa kuchukuwa ardhi yao ambapo kesho wanakusudia kufungua kesi Mahakama ya Ardhi dhidi yake kwa msaada wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Kulia ni mkazi wa kijiji hicho, Jimmy Mwasenga na Mwangalizi wa LHRC, Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena.![]()
Mwangalizi wa LHRC, Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu mgogoro wa ardhi dhidi mwekezaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya Union ambaye anadaiwa kuchukuwa ardhi yao ambapo kesho wanakusudia kufungua kesi Mahakama ya Ardhi dhidi yake kwa msaada wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Kulia ni mkazi wa kijiji hicho, Jimmy Mwasenga.
Mkazi wa Kijiji cha Chiwachiwa, Comrade Mlonganile (kulia), akizungumza katika mkutano huio wakati akichangia jambo. Kushoto ni Zabron Mpwage mmoja wa wanakijiji hicho.
Mkazi wa Kijiji hicho, Jimmy Mwasenga (kulia), akichangia jambo.
Wawakilishi wa kijiji hicho wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Zabron Mpwage, Comrade Mlonganile, Raina Ngapya, Mwangalizi wa Haki za Binadamu LHRC Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena, Merkizedek Mazani na Jimmy Mwasenga.
Na Dotto Mwaibale.
WANANCHI wa Kijiji cha Chiwachiwa kilichopo Tarafa Mgeta Kata ya Mbingu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kesho wanakusudia kufungua kesi Mahakama ya Ardhi dhidi ya Kampuni ya Usafirishaji ya Union kwa madai ya kuchukua ardhi yao kesi ambayo itasimamiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwangalizi wa Haki za Binadamu wa LHRC, Godfrey Lwena alisema kesi hiyo wanatarajia kuifunga kesho baada ya kupokea malalamiko ya wanakijiji hicho.
"Baada ya kupokea malalamiko ya wanakijiji hicho chenye kaya 850 tulikwenda Halmshauri ya Wilaya ya Kilombero kujua mmiliki halali wa maeneo ya kijiji hicho ambapo uongozi wa wilaya hiyo ulishindwa kutoa vielelezo vinavyoonesha umiliki halali wa mwekezaji huyo.
Mkazi wa kijiji hicho Merkizedek Mazani alisema wameanza kuishi eneo hilo tangu miaka 1974 na hawakuwahi kumuona mwekezaji yeyote wanashangaa wanapoambiwa eneo la kijiji hicho ni mali ya mwekezaji huyo hivyo waondoke.
Aliongeza kuwa katika kijiji hicho kunamiundombinu ya barabara, shule ya msingi ambayo imesajiliwa kwa namba MG/05/021/142 na kuwa na kijiji hicho kilitangwazwa na Serikali kuwa kijiji kwa tangazo namba 180/2010.
Aliongeza kuwa hivi sasa katika kijiji hicho hakuna shughuli zozote za serikali zinazo fanyika kwa kuwa hawakufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kutokana na mgogoro huo.
Mazani alisema kwa mihula mitatu walifanya uchaguzi wa viongozi wao bila ya kuwa na zuio lolote lakini wanashangaa kuzuiliwa kufanya uchaguzi huo kwa barua yenye kumbukumbu namba KDC/E.30/5/VOL.VI/24 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa wilaya hiyo wakidai kijiji hicho kutotambuliwa.
Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Anzimina Mbilinyi alipopigiwa simu jana ilikutaka kutoa ufafanuzi wa madai hayo alituma ujumbe mfupi wa simu yake ya mkono kuwa hakuwa katika nafasi nzuri ya kuongea na simu.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Hassan Masalla alisema anaomba apate muda wa kuwasiliana na wenzake ili apate majibu ya uhakika ya kujibu kwani halikuwa hajui chochote kuhusu madai hayo.
Hata hivyo jitihada za kumpata mwekezaji huyo ili kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa.
↧
AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SECONDARY NANJ MONDULI ARUSHA
Wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja wakionyesha vitabu vyao mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha. wakishuhudia ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha wakishuhudia kulia ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nanja Yona Lukas.
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akipitia kitabu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu.
Na Mwandishi Wetu.
*Chini ya mpango wake wa shule yetu, shule za sekondari manyara, Moshi na Tanga kupokea msaada huo mwenzi huu
Wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Nanja wamepokea msaada wa vitabu kutoka Airtel, Msaada utakaoweza kuchangia katika kutatua tatizo la uhaba wa vitabu shule ni hapo.
Akitoa taarifa ya shule , Mkuu wa shule ya sekondari ya Nanja Bwana Yona luka alisema” shule yetu ina jumla ya wanafunzi 549 na walimu 32, matokeo ya shule ya kidato cha nne yanakuwa kila mwaka ufaulu wa asilimia 71% pamoja na kukua kwa kiwango cha ufaulu bado shule inachangamoto nyingi ikiwemo uhaba wa vitabu na walimu.
Kwa sasa uwiano wa vitabu vya sayansi ni kitabu 1 kwa wanafunzi 5 wakati kwa vitabu vya sayansi ya jamii uwiano ni kitabu 1 wanafunzi 30. Tunafurahi sana kupokea vitabu hivi toka Airtel kwani msaada huu umekuja kwa wakati muafaka”
Akiongea wakati halfa hiyo fupi ya kukabithi vitabu , Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya alisema” napenda kuwashukuru sana Airtel kwa kufikisha msaada huu wa vitabu kwa sekondari hii ya Naja, vitabu hivi vya sayansi havitachangia kuongeza kiwango cha ufaulu tu bali vitawahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi.
Natoa wito kwa walimu kuwapatia wanafunzi vitabu hivi wavisoma ili kuwajengea wanafunzi hawa tabia ya kusoma vitabu. Nawahasa wanafunzi kuvitunza vitabu ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi shuleni hapa.
Aliongeza kwa kusema” shule imeweza kujenga maktaba lakini tunayochangamoto ya uhaba wa vifaa vya maktaba , nachukua fulsa hii kuwaomba Airtel waendelee kutusaidia kwa kuchangia vifaa vya mahabara na kuwezesha masomo ya sayansi ya vitendo”
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja wa kanda ya kaskazini Brighton Majwala alisema”wote tunatambua tatizo la uhaba wa vitabu katika shule za sekondari ambapo hali halisi haiendani namahitaji, uwiano wa kitabu 1 ni kwa wanafunzi 10.
Kwa kuliona hilo Airtel tumejikita na kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunatutua changamoto hii na kuongeza kiwango cha ubora wa elimu nchini. Natoa wito kwa wanafunzi wa Nyala kuzitumia vitabu hivi vizuri na kuboresha kiwango cha ufaulu.
Kwa upande wa wanafunzi wameishukuru Airtel kwa kuboresha elimu na kusema vitabu hivi vitawasaidia kuongeza ujuzi katika masomo ya sayansi na kufanya vizuri zaidi.
↧
KATUNI YA LEO
↧
↧
RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE JIJINI PARIS
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Ikulu ya Ufaransa maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015 kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande katika Ikulu ya Ufaransa maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande Ikulu ya Ufaransa maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015 kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande.
PICHA NA IKULU
↧
DC MJEMA APONGEZA UONGOZI WA TWAYYAIBAT ISMLAMIC SEC KWA KUPUGUZA ADA
Wadau wa Elimu, Abdulaziz Jaar kulia, akizungumza jambo katika matembezi ya Shule ya Kiislamu ya Twayyibat Islamic Seminary ya Temeke jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau kutoka Yukubu Chamber&Associate.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya Temeke, DC Sophia Mjema, ameipongeza shule ya Sekondari ya Kiislamu yojulikana kama Twayyaibat Islamic Seminary Secondary School kwa kufanya ada nafuu inayoweza kuwafanya wazazi na walezi wamudu gharama za kusomesha watoto kwenye shule binafsi.
mwanafunzi kutoka Twayyibat Islamic Seminari akisoma Quraan katika shule hiyo walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, hayupo pichani.
DC Mjema aliyasema hayo alipofanya ziara katika shule hiyo na kukuta uongozi wa Twayyaibat, ukitoa ada ya Sh 200,000 tu kwa mwaka, jambo ambalo ni agharabu mno hususan kwa shule za kulipia na zinazomilikiwa na taasisi za kidini.
Akizungumza kwa mshangao mkubwa mbele ya wadau wa elimu, DC Mjema alisema ameshangazwa na shule hiyo kufanya ada nafuu, hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kujitokeza kuwasomesha watoto wao kwa nguvu zote.
Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Skywadrs Construction, Saeed Pirbaksh Mulla, akipokea cheti cha kutambua mchango wa kampuni yao kwenye shule hiyo. Cheti hicho anakabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia.
Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango cha juu.
“Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.
“Naomba wadau, walezi, wazazi na serikali kupanga namna wanavyoweza kuisaidia Twayyaibat ili waweze kuhakikisha kuwa vijana wetu wanasoma kwa bidii kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kwasababu Dunia ya leo elimu ni lazima,” alisema DC Mjema.
Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, alisema shule yao imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto wanaosoma kwenye shule hiyo.
“Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi,” alisema.
Katika hatua nyingine, DC Mjema alitumia muda huo kukabidhi vyeti vya kuthamini mchango wa wadau wanaoisaidia shule hiyo, huku waliopewa vyeti hivyo ni Skywards Construction, Yakubu Chamber&Associate, Mheshimiwa Adam Malima, Sheimar Kweigir, Zainabu Vulu, Alosco.
Kazumari Nambeya, akiiwakilisha Home Shooping Centre katika kupokea cheti cha kutambua mchango wa shule hiyo, mbele ya Mkuu wa wilaya Temeke, Sofia Mjema, jana, jijini Dar es Salaam.
Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango cha juu.
“Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.
“Naomba wadau, walezi, wazazi na serikali kupanga namna wanavyoweza kuisaidia Twayyaibat ili waweze kuhakikisha kuwa vijana wetu wanasoma kwa bidii kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kwasababu Dunia ya leo elimu ni lazima,” alisema DC Mjema.
Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, alisema shule yao imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto wanaosoma kwenye shule hiyo.
“Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi,” alisema.
Katika hatua nyingine, DC Mjema alitumia muda huo kukabidhi vyeti vya kuthamini mchango wa wadau wanaoisaidia shule hiyo, huku waliopewa vyeti hivyo ni Skywards Construction, Yakubu Chamber&Associate, Mheshimiwa Adam Malima, Sheimar Kweigir, Zainabu Vulu, Alosco.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza na wanafunzi na wadau wa shule ya Twayyibat, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa elimu na wasaidizi wa shule ya Twayyibat Islamic, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.
↧
DOG WHISPERER: TRAINER WALKS PACK OF DOGS WITHOUT A LEASH
↧
ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC GEITA NA KAGERA YAHAMASISHA MAENDELEO
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw. Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili kuvutia na kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania na Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC na baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu mwaka 1978. NHC iliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kulirejeshea eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akimpa maelezo Mjumbe wa Bodi ya NHC Bi Subira Mchumo ya juhudi zinazofanywa na NHC katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya nchini za kuwapatia wananchi makazi bora. Ujumbe huo ulitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba na kusisitiza matumizi ya malighafi zinazopatikana katika maeneo husika ili kupunguza gharama za nyumba hizo.![]()

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika Wilaya ya Muleba kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho ya ukamilishaji.
Msanifu wa Majengo wa NHC Bw. Kintu akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ya jengo linalojengwa na NHC eneo la Mtukula ili kukuza biashara upande wa Tanzania.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ulipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kujionea juhudi zinazofanywa na mwekezaji wa kiwanda hicho katika kutoa ajira kwa watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Kiongozi wa kikundi cha vijana kilichoko Wilaya ya Bukoba Mjini waliyofadhiliwa na NHC mashine za kutengezea matofali ili kujipatia ajira
↧
↧
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AZURU KABURI LA ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS HAYATI DR.OMAR ALI JUMA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni wakati alipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais Hayati Dr. Omar Ali Juma aliyefariki mwaka 2001 katika kijiji cha cha Wawi Mchekeni wilaya ya Chakechako mkoa wa Kusini Pemba leo, katikati ni MNEC wa wilaya ya Chakechake Bw. Daud Ismail.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakiomba dua wakati Katibu Mkuu huyo na msafara wake walipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais Hayati Dr. Omar Ali Juma.

Baadhi ya viongozi wanawake nao wakijumuika kuomba dua.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa kahawa na baadhi ya viongozi kutoka kulia ni Balozi Ali Karume mjumbe wa halmashari kuu ya Taifa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Mzee Ali Abdalla Ali. Picha na John Bukuku.
↧
WEUSI, BEN POL, GRACE MATATA NA MROSHO MPOTO WAONGEZEKA KUTOA BURUDANI MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA THT
• Viingilio shilingi elfu 15 kwenye vituo na elfu 20 mlangoni
Tamasha la miaka kumi ya THT litakalofanyika jumamosi hii katika viwanja vya Escape 1 Mikocheni, limekamilisha maandalizi yake na hivyo kuwataka wadau na wapenzi wake wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani kubwa ya mziki hapa nchini.
THT, ambayo inasifika kwa kuzalisha wasanii mahiri nchini kama Linah, Barnaba, Mwasiti, Ditto, Mataluma, Vumi, Beka, Recho, Marlaw, Msami, Makomando na wengine wengi, imejipanga kutoa burudani kubwa ya mziki kwa mashabiki wake.
Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa THT, Mwita Mwaikenda alisema maandalizi yanaenda vema na mashabiki wahudhurie kwa wingi kujionea namna kituo hicho kilivyoweza kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya muziki.
‘Mpaka sasa wasanii wa THT watakaotoa burudani wako tayari, na kama mnavyojua THT utamaduni wake ni kupiga muziki kwa kutumia bendi lakini pia wasanii watakaotusindikiza ni kama Ben Paul, Mrisho Mpoto na Weusi’ alisema Mwita.
Akizungumzia wadhamini waliojitokeza kwenye shughuli hiyo, Mwita aliwashukuru Mr. Price waliowavisha wasanii wote, Mziiki.Com ya Spice Afrika walionunua tiketi 500 za tamasha kwa ajili ya wateja wao, SanMoto Pikipiki waliotoa pikipiki, Tanzania Fashion and Design Limited, Darling Hair ambao wametoa nywele kwa waimbaji wote wa kike na Clouds Media Group.
‘Tunatoa shukrani za dhati kwa wadhamini wetu, kwa kutuunga mkono katika kuadhimisha miaka kumi ya kuleta mapinduzi katika burudani’ alisema Mwita.
Tiketi za tamasha zinapatikana maduka ya Robby One Fashion Kinondoni na Sinza, Yahya Boutique Kinondoni, Born 2 Shine Mwenge, Ofisi za Clouds, Moca City Samora Avenue, City Sports Lounge, Mr Price na THT Kinondoni.
Kiingilio ni 15,000/- kwenye vituo hivyo na kwa wale wanaotaka za VIP ni 50,000/- na zinapatikana THT pekee yake. Siku ya onyesho pale Escape One, mlangoni kiingilio kitakuwa ni Shs 20,000/=.
↧
RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na balozi wa New Zealand nchini Ufaransa baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ni ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwakilishi wa ubalozi wa Uganda nchini Uraransa baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. Ubalozi wa Tanzania ulikuwa katika majengo ya ubalozi wa Uganda kabla ya New Zealand kuiuizia anzania majengo hayo ambayo
ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua na kuweka saini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa
ubalozi.
ubalozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijichanganya na wageni waalikwa ambao ni mabalozi wa nchi mba,limbali za Afrika pamoja na wana Jumuiya ya Watanzania baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
PICHA NA IKULU
PICHA NA IKULU
↧