Wanamasumbwi leo kwa uchache walijikusanya katika viwanja vya leaders na kukipiga mechi ya kirafiki ya kudumisha uhusiano mzuri baina yao. Mechi hiyo ambayo iliandaliwa kimzaha huku baadhia ya wanamasumbwi wakiwa hawana taarifa ya mchezo huo walikurupuana asubuhi na kucheza mechi hiyo bila wasiwasi kana kwamba mpira wanaujua.
Kipindi cha pili timu zote zilijipanga vizuri na hazikuweza kufungana huku mpira ukiiisha huku timu ya mabondia ikitoka na bao moja kwa moja na Timu ya Taswa (waandishi wa Habari). Timu hizo zimepanga yafanyike marudiano ilikuweza kumbaini mshindi.