Moja ya mambo ambayo hayapaswi kufumbiwa macho ni suala la maeneo sahihi ya kufanyia biashara, napenda kutoa masikitiko yangu kwa manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kuendelea kufumbia macho kituo cha mabasi madogo ya Mwenge, Dar es Salaam kwa kukihalalisha kuwa ni gulio la nguo. Ni mara nyingi jambo hili limekuwa likipigiwa kelele ila wahusika naona wameamua kufumbia macho kwa kuendelea kuchukua ushuru kwa wafanyabishara hawa na kuwaacha hapa. Swali la kujiuliza je hiki ni kituo cha daladala au gulio la nguo??? Wahusika naomba wananchi tupate majibu maana kuendelea kufumbia macho wafanyabishara hawa kunaendelea kukuza wizi na unyang'anyi wa kila siku katika eneo hili.
Akinadada wakiendelea kuchagua nguo zilizokuwa zikiuzwa.
Biashara ikiendelea kupamba moto.