Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

CCM WAKATAA DARAJA LA RAU LILILOJENGWA NA MANISPAA KWA TSHS. MILIONI 102

$
0
0
Sehemu la Daraja la Rau, lililoko katika manispaa ya Moshi, Mkoani Kiliamnajro lililokataliwa na Viopngozi wa CCM wilaya ya Moshi katika ziara ya kukagua miradi ya manispaa Moshi ili kujiridhisha kama miradi inayoendeshwa na Manispaa hiyo ianendena na kiwango kinachotakiwa.

Katibu wa CCM, Aluu Segamaba akiongoza viongozi wenzake kukagua daraja la Rau linadaiwa kujengwa kwa kutumia kiasi cha sh. milioni 102, lililokatika kabla ya ujenzi wake kukamilika, viongozi wamelikataa daraja hilo.

Daraja la Rau lililojengwa na Manispaa ya Moshi na kukataliwa na timu ya Viongozi wa CCM wa wilaya hiyo katika Ziara ya kukagua miradi ya serikali inayotekelezwa na Manispaa hiyo.
---
Na Mwandishi Wetu Moshi

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi, imelikataa daraja la manispaa iliyojengwa katika kata ya Rau mbokomu lililojengwa kwa kutumia fedha za serikali kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ujenzi wake.

Wakizungumza baada ya kukagua daraja hilo, ambalo pamoja na ujenzi wake kutokamilika na kukabidhiwa kwa wananchi, Viongozi wa CCM wilayani hapa ambao walikuwa katika ziara maalum ya kukagua miradi ya serakili iliyojengwa katika manispaa hiyo, walisema inasikitisha kuona kazi muhimu kama ujenzi wa daraja likitekelezwa kizembe.

Viongozi hao kutoka katika Kamati ya Siadsa ya Halmashauri kuu CCM wilaya ya na Sekreteriet ya Halmashauri kuu ya CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Mkutano mkuu CCM Taifa, Aggrey Marealle, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi, Elizabeth Minden a Katibu wa CCM wilaya, Aluu Segamba wamelikataa daraja hilo kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.

Wakiwa wameongozana na Mkadiriaji wa Gharama za ujenzi wa Manispaa , Mhandisi Charles Huka na Msaidizi wa Mchumi wa Manispaa, Evera Lyimo. Viongozi hao walisema hata kiasi cha fedha cha sh. Milioni 102, kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo lililoanza kubomoka hata kabla ya ujenzi wake kukamilika ni kidogo mno ikilinganishwa na ukubwa wa kazi.

Akizungumza kuhusu tamko lao, katibu wa CCM wilaya ya Moshi, Aluu Segamba alisema kimsingi wao kama chama tawala, hawajaridhika na kiwango cha ujenzi wa daraja hilo huku akiwataka wananchi kutopitisha magari yao katika daraja hilo kwa usalama wao na kuongeza kuwa ujenzi huo unatakiwa urudiwe upya.

Alisema kuwa kilichofanyika katika daraja hilo ni uhuni mtupu na kuongeza kuwa hawatakubali kuona fehda za umma zikiteketea ovyo kutokana na uzembe wa watu wachache.

“Kimsingi hili daraja hatujaridhika na kiwango cha ujenzi wake, huu ni uhuni na kamwe kama chama tawala hatuwezi kukaa kimya huku fedha za umma zikitafunwa kizembe, utajengaje daraja kwa kutumia milioni 102? Tunawaomba wananchi wasipitishe magari hapa hadi litengezwe katika kiwango kinachoridhisha,”alisema Segamba.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>