Leo nasherekea siku yangu ya kuzaliwa (birthday) 15. 5 nilizaliwa majira ya saa saa 5 asbh, dah! imeangukia siku nzuri sana yaani 15/5 /siku ya jumatano saa tano kamili asbh. Eeeh Mungu naomba uendelee kunijaalia yote yalio mema uniongoze, unilinde mimi na familia yangu, ndugu zangu, majirani zangu, marafiki zangu, wasanii mwenzangu, viongozi wangu, nchi yangu kwa ujumla, na unizidishie marafiki wema, wakweli, wenye kuniambia ukweli pale ninapokosea na hata kunipongeza pale nilipopatia.
Namkumbuka sana Shangazi yangu kipenzi (Asha khariki nyange ) nilikupenda sana na nitazidi kukupenda daima, huwa naumia mno kukukosa ila sina la kufanya zaidi ya kukuombea dua tu inshaallah Mungu akuangazie. Eeeh Mungu tazama hata ndoto zangu ni kubwa sana kibinaadam lakini kwako ni ndogo mno. Eeeh mola Wangu naomba zifanikishe zote zitimie naamini kwako hakuna lishindikanalo.
Wapendwa tupendane tuombeane kheri na baraka, Nawatakia kheri na mafanikio nawapenda sana sana sana.
Imetolewa na Mwanaisha Sady Nyange (Dayna nyange).