
Uzinduzi wa Video hiyo ambao umeandaliwa na Kampuni ya Yuneda Entertainment inayohusika na masuala ya burudani itawapambanisha wasanii hao ambao kutatafutwa nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo nyimbo hiyo ya muziki gani inamahadhi ya kubishana kati ya miziki hiyo.

"Onesho hili litakuwa ni la kumtafuta nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo kupitia uzinduzi wa video hii utadhihirisha nani mkali kati ya muziki wa bongo fleva na hip hop,"alisema Mwendesha.
Alisema mara baada ya video hiyo kuzinduliwa Mei 18 Dar LIVE uzinduzi huo utahahamia katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza, na baadaye Arusha na kuwataka mashabiki wa mikoa hiyo kukaa tayari kwa ajili ya burudani hiyo.