Na Mwandishi wetu
TIMU ya Foosball ya Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper(TSN) juzi imetinga hatua ya fainali baada ya kuzishinda timu nyingine tano zinazowakilisha vyombo mbalimbali vya habari katika ligi ya mchezo huo inaoendelea.
Mpambano wa Mchuano wa Foosball kati ya timu ya Kajunason ambayo iliundwa na mmiliki wa blogu hii, Cathbert Angelo (kulia) akiwa na Seif Kabelele ilichuana vikali na timu ya Times Fm iliyoindwa na Ndimbo. Ambapo katika mchuano huo timu ya Times Fm walishinda na kusonga mbele.
Baada ya Times Fm kushinda ndiyo walipokutana na vijana wa timu ya Gazeti la Majira (kulia) ambao waliwagalagaza na kuwatoa nje ya mashindano.
TSN iliyowakilishwa na wachezaji wake Masembe Tambwe na Oscar Job, ilifanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuzifunga timu za Kajunason Blog, Majira, Mtanzania, Dira ya Mtanzania, Channel Ten pamoja na timu ya Tanzania Daima na hivyo kujinyakulia jumla ya pointi kumi kulingana na taratibu za mashindano hayo.
Fainali za foosball zinatarajiwa kufanyika Mei 25 katika Hotel ya Golden Tulip Jijini Dar es salaam, ambapo TSN, timu zingine saba zilizoingia hatua hiyo
pamoja zingine zinazotarajiwa kupatikana katika mikoa ya Arusha na Mwanza zitachuana kupata timu moja itakayosafiri kwenda mji wa Amsterdam, Uholanzi yalipo makao makuu ya wadhamini wa mchezo huyo kampuni ya Heinkein.
...hatimaye timu ya Gazeti la Majira nayo iliingia uwanjani kutetea ubingwa wake pale ilipokutana na timu ya Gazeti la Nipashe (kushoto) ambao waliwatoa nje na kufanya timu ya Gazeti la Nipashe kusonga mbele.
...nikipata chakula pamoja na Sharon mara baada ya kutoka kwenye mpambano wa Foosball.
Katika mchezo huo uliochezwa katika mgahawa wa Ambassador uliopo katikati ya Jiji la Dar es salaam, timu ya TSN ilionyesha uwezo mkubwa huku ikishinda idadi nyingi ya magori dhidi ya timu zote tano ilizoshindana nazo.
Akizungumza mashindano hayo ya jana, Meneja wa Heinkein Tanzania Uche Unigwe, mbali na kuzipongeza timu zilizoshiriki, alisifu kiwango kilichonyeshwa na wachezaji wote wa TSN huku akiwataka kujiandaa katika mchuano utakaowakutanisha wao kwa wao ambapo mshindi ataungana na washindi wawili kutoka timu zingine kwenda Uholanzi.
Wanahabari wakifurahia pamoja mara baada ya mchuano wa mchezo wa Foosball.
Timu ya vijana wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper (TSN) ikiongozwa na Tambwe na Oscar Job walipokutana na vijana wa timu ya Gazeti la Dira ya Mtanzania (kulia) ambao waliwagalagaza na kuwatoa nje ya mashindano.
Mshereheshaji wa mchezo huo, Msanii Cpwaa akijaribu kuchombeza wakati mchuani wa mchezo wa Foosball ukiendelea.
Timu ya Mtanzania nayo iliweza kuonyesha makali yake japo hawakufua dafu kwa Timu ya vijana wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper (TSN) ikiongozwa na Tambwe na Oscar Job.
Aha! vijana wa Timu ya vijana wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper (TSN) ikiongozwa na Tambwe na Oscar Job waliwanyuka tena timu ya Channel Ten.
Mashabiki ambao ni wanahabari wakifuatilia.
Baadae timu ya Gazeti la Majira ilirudi uwanjani kutetea ubigwa wake kwa kucheza fainali na timu ya vijana wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper (TSN) ikiongozwa na Tambwe na Oscar Job ambao walishinda na kujikuta wakichukua ubingwa huo.
Mshereheshaji wa Michuano hiyo ya Foosball, Msanii Cpwaa akiitangaza Timu ya vijana wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper (TSN) ikiongozwa na Tambwe na Oscar Job.
Wakipewa zawadi na Afisa masoko wa Heineken Tanzania, Caroline.
Mchezaji wa Timu ya vijana wa Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standards Newspaper (TSN) ikiongozwa Oscar Job akipokea zawadi zake mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi.
“Ni michuano mipya hapa nchini, sikutarajia kuona uwezo mkubwa kama huu kutoka kwa waandishi wa habari kutokana na majukumu yao mengi katika uhabalishaji, matarajio timu zote zilizoshiriki zitaendelea kujinoa kwa ajili ya mashindano mengine msimu ujao” alisema Unigwe.
Wakizungumzia ushindi walioupata wachezaji wa TSN Job na Tambwe kwa pamoja walisema hatua hiyo imetokana na kujituma kwao kama timu walipokuwa wakicheza hali iliyowasaidia kuwakabili vizuri wapinzani wao.
Hadi sasa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali za mchezo wa Foosball uliozinduliwa Machi 13 Mwaka huu na Baa zinapotokea ni pamoja na ‘Yellow Tables’(Jackies),Manu (Didis), Bolingo(Corner Bar), Masters ( Masaki), Bolbusters(Samaki samaki ,Mbezi), Airtel (Copa Cabana) na timu ya Bizzo inayowakilisha baa ya Kisuma.