Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

SERIKALI YA TANZANIA YAWASILISHA MABORESHO MAENDELEO

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania ukuiwasilisha mpango wa maboresho ya maendeleo kwa Benki ya Dunia. Mpango huo unahusu maendeo katika maeneo ya Elimu, Maji, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo na Usafirishaji.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho katika Elimu, Maji, Nishati, Usafirishaji, Rasilimali Fedha na Kilimo.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia katikati akifafanua jambo wakati wa majadiliano, kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akifafanua jambo katika majadiliano hayo.
Ujumbe kutoka Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Dr. Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho hayo.
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Dr.Mpango akijibu hoja mara baada ya kuwasilisha mpango wa maboresho. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile na Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka.

Habari na Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC
---
Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria mikutano ya majira ya kipupwe mjini Washington DC wapata fursa ya kufanya majadiliano na timu nzima ya Benki ya Dunia kuhusu namna ya kuleta maendelea ya haraka. Majadiliano haya yaliwasilishwa na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango ambaye aliwasilisha vyema mkakati mpya wa Big Results Now.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile alisema kuwa fursa waliyoipata imewawezesha kuelezea mpango huu mpya ambao utatuletea matokeo makubwa na ya haraka hivyo walimwomba, Dr. Mpango aelezee msukumo mzima wa mpango huo. 

Katika kuwasilisha mpango huo, Dr. Mpango alisema kuwa mfumo huu mpya ambao Serikali yetu imeamua kuufanya utaboresha upya utendaji kazi ndani ya Serikali. ”Tumeamua kuanza na maeneo muhimu sita ambayo ni kilimo, usafirishaji, nishati, maji, elimu na rasilimali fedha.” Alisisitiza Mpango.

“Kwa upande wa usafirishaji serikali itahakikisha bandari ya Dar es Salaam, reli ya kati pamoja na barabara za ukanda wa kati zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi”. Aliongeza Mpango. Akizungumzia nishati alifafanua kuwa lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha kwamba tatizo la umeme linatatuliwa kwa haraka ili kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi wenye kasi zaidi. Kwa upande wa suala la maji nalo halikuachwa nyuma kwani kwa sasa maji ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu walioko vijijini .Alisema Mpango.

“Kwa upande wa Elimu Serikali imedhamiria kupitia utaratibu huu wa matokeo makubwa sasa ili ilete mabadiliko ya haraka kutoka asilimia 41 nakufikia asilimia 60 kwa mwaka 2013 na hatimaye kufikia asilimia 80 ya kiwango cha ufaulu kwa miaka mitatu ijayo yaani kufikia mwaka 2015. Eneo la rasilimali fedha ambazo zitaweza kusaidia katika maeneo haya tuliwaeleza mbinu ambazo zitaibua vyanzo vipya vya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi lakini pia namna bora zaidi yakutumia sekta binafsi ili kusaidia Serikali” Alisema Mpango.

“Jambo la kujivunia katika hili ni kwamba utaratibu huu ni wa kwetu wenyewe na serikali ndio imebuni na kuanza kuutekeleza sisi wenyewe, sio jambo ambalo tumesukumwa na wafadhili, bali viongozi wetu wameusimamia ili uweze kufanikiwa na hatimaye wananchi waweze kupata maisha bora zaidi.” Alisema Mpango.

Benki ya Dunia kwa kuona umuhimu wa mpango huu wameonyesha maeneo ambayo serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha kwamba mfumo huu unafanikiwa.

Kwa kuhitimisha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. S. Likwelile alisema kuwa “Benki ya Dunia imeunga mkono jitihada hizi na kwamba rasilimali chache tulizonazo zitatuwezesha kuzaa matunda na kwamba watafanya kazi pamoja na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba mipango yote tunayofanya ielekezwe katika kuzaa matunda katika Elimu, Nishati, Usafirishaji, Kilimo, Maji na Rasilimali Fedha. Na kikubwa walichosisitiza ni suala la uwazi na namna gani raia wa kawaida anaweza kushirikishwa katika kutoa maoni yao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>