Miss Utalii Tanzania wakifurahi wakati wa mazoezi katika Fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan.
Mhifadhi Utalii Emmanue Njiku, wa hifadhi ya Sadaan akifafanua jambo kwa Miss Utalii Tz 2013 wakati wa ziara hivi karibuni.
Washishiriki Miss Utalii Tanzania 2013-katika ziara ya mafunzo mto Wami- walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan Juzi.
Miss Utalii Tz wakiwa katika pozi katika Milima ya Udzungwa.
---
Miss Utalii Tanzania ivi sasa wako katika ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa za Utalii ikiwa ni katika kujifunza vitu mbalimbali kuelekea Fainali kuu ya Taifa ambayo itapangwa baada ya kushindwa kufanyika kwa kuwa washiriki walikuwa katika matembezi ya kutembelea hifadhi katika Mto huo.
Mpaka sasa washiriki hawa wametembelea hifadhi za Taifa za Saadan ambako walijionea Utalii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ule wa Kutumia Boti nkatika Mto Wami ambako waliweza kushuhudia Viboko na Mamba wengi wakiwa katika mto huo, aida katika hifadhi ya Taifa ya Sadani pia waliweza kufanya Onyesho la kutafuta Tuzo ya Utalii wa Ndani ambapo Miss Utalii Mkoa wa Arusha aliibuka mshindi.
Baada ya onyesho hilo Saadan washiriki Miss Utalii Tanzania 2013 walitembelea hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ambako walifanikiwa kupanda katika Milima hiyo na kufanikiwa kutazama kivutio kikubwa cha Maporomoko ya maji kwenye Mlima wa Mlima Sanje.
Aidha baada ya kujifunza kutoka katika maporomoko hayo washiriki wa Miss Utalii Tanzania walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Mikumi ambako wamejionea Wanyama mbalimbali wakiwemo Simba, makundi ya Nyati, Makundi ya Tembo, na Swala.
Hata hivyo kabla ya kuondoka katika hifadhi ya Mikumi wanatarajia kufanya onyesho kwa ajili kupata mwakilishi wa tuzo ya Tanapa na ile ya utalii wa ndani kabla ya kuelekea mlima kilimanjaro na hifadhi zingine.
Kambi ya Miss Utalii ambayo imeanza upya baada ya kuvunjwa kutokana na Washiriki wengi kwenda katika mitiani ya vyuo inatarajia kupanga ratiba ya Fainali hizo baada ya washiriki wote kuwasili kambini.