Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imedhamini Mbio za Sita za Ngorongoro Marathon zenye lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria zinazotarajiwa ‘kutimua vumbi’ jumamosi ya Aprili 6, mwaka huu katika mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha. Ufunguzi wa mbio hizo utafanywa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.
Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kuwa, kwa mwaka huu kampuni hiyo imetoa fedha taslimu, simu za kisasa kabisa za mkonaoni pamoja na muda wa hewani kwa mshindi wa kwanza wa kundi la wanaume na mshindi wa kwanza kwa kundi la wanawake.
“Tigo kwa kuwajali Watanzania, tumeona umuhimu mkubwa sana wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambapo dhidi ya malaria ambayo imekuwa ikipoteza maisha ya watu wengi wa rika mbalimbali kupitia mbio hizi…” alifafnua Mpinga.
Kwa upande wake Mratibu wa ZARA Charity ambao ndio waandaji wa mbio hizo Bw, Datus Joseph alifafanua kuwa, pamoja na kusaidia mapambano dhidi ya malaria, mbio za Ngorongoro Marathon pia zinasaidia kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi.
“Mbio hizi ni za Sita tangu kuanzishwa kwake na Tigo wameendeea kutupa ‘support’ na tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa wadhamini wetu…” alifafanua Joseph.
Aliendelea kufafanua kuwa, ZARA Charity inawashukuru wadhamini mbalimbali wa mbio hizo ambazo zimekuwa za mafaniko makubwa