Kijana fundi seremala ambae pia alichonga jeneza la marehemu Bw Solomon a.k.a Baba akiliweka wakifu kaburi kwa kulimwangia mchanga ambao yeye alidai ni maji ya uzima. Baadhi ya waombolezaji wa msiba huo wakiwa wamekata tamaa baada ya katekista kuingia mitini leo. Hapa mhubiri wa kujitolea akiongoza ibada ya mazishi kwa kutoa neno. Mwili wa marehemu Rejina Lweve ukiwa makaburini
Baadhi ya waombolezaji wa msiba wa Bi Rejina Lweve mkazi wa Kihesa katika Manispaa ya Iringa wameeleza kusikitishwa kwao na udanganyifu uliofanywa na mmoja kati ya makatekista wa RC eneo la Mgongo baada ya mtumishi huyo wa Mungu kudaiwa kutumia lugha ya udanganyifu kukwepa kuongoza idaba ya mazishi kwa madai kuwa anakwenda kutafuta maji ya uzima.
Tukio hilo lilionyesha kuwakwaza zaidi waombolezaji hao na kupelekea baadhi yao kuamua kuondoka kabla ya shughuli za mazishi kufanyika.
Wakizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya waombolezaji walisema kuwa hawajapendezwa na hatua ya kiongozi huyo wa kidini kususia kuongoza ibada hiyo na kuwa kufanya hivyo ni kushusha heshima la kanisa hilo la RC ambalo linaheshimika zaidi duniani .
Hivyo wamemwomba askofu wa kanisa hilo mkoani Iringa kulitazama kwa kina suala hilo ili ikiwezekana kuwaondoa watendaji kazi wa parokia na vigango ambao wanatabia kama hizo za kusisia maiti.
Pia walisema kuwa kateksta huyo aliaga kuwa anakwenda kufuata maji ya uzima nyumbani kwake ila toka alipoondoka mida ya saa 8 hakuweza kurejea tena hadi saa 10 jioni walipoamua kumtuma dereva wa boda boda kumfuata bila mafanikio na kulazimika kumwomba mchonga majeneza Kihesa ili kuendesha idaba hiyo.

SHUKRANI ZA DHATI: Francisgodwin Blog.