KUTOKANA na ushirikishwaji mdogo wa vijana katika shughuli za kimaendeleo Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (YUNA) imeandaa mkutano wa baraza kivuli la kimataifa la Umoja wa Mataifa litakalo jadili na kupendekeza masuluhisho ya matatizo mbalimbali ya dunia
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa Asasi hiyo Lwidiko Mhamilawa alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kusaidia vijana na kuonyesha umuhimu wa vijana katika ukusanyaji wa maoni utakao changia maendeleo kwa taifa
Alisema kuwa katika mkutano huo ambao unatarajiwa kuanza tarehe mbili mwezi wa nne utakuwa na mada kuu nne ambazo ni pamoja na kutafuta suluhu ya afya na magonjwa, mabadiliko ya tabia ya nchi, amani pamoja na maswala ya nishati
Alieleza kuwa washiriki wa mkutano huo hufanya tafiti kuhusu nchi mbalimbali hupata majukumu kama yale ya wanadiplomasia hujadili, huelimisha na kushauriana nini kifanyike hatimaye kupendekeza masuluhisho ya matatizo mbalimbali ya dunia`
"Mkutano huu unalengo kuu kumsaidia kijana kujiona ni sehemu ya maendeleo, na kujichukulia ni sehemu ya mabadiliko katika jamii yetu na asisubili afanyiwe anatakiwa yeye afanye " alisema Mhamilawa
Aliongezea kuwa katika mikutano iliyopita walipendekeza elimu ya ujasiriamali uingizwe kwatika mfumo rasmi ili iweze kuwasaidia vijana wengi kujiajili na pindi wamalizapo masomo yao na si kungoja kuajiliwa kama ilivyozoeleka
Mkutano huo umekuwa ukianadaliwa kwa miaka 15 mfululizo ambapo kwa mwaka huu nchi ya Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano huo unaotalajiwa kufanyika mkoani Dodoma.