Waziri wa Utalii, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Said Ali Mbarouk akikata utepe kuashiria kuzindua duka la Zantel lilopo eneo la Muzamil, Zanzibar. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Next Telecom, Zanzibar Bw. Mohamed Chanja.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Zanzibar Bw. Mohamed Mussa (katikati) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa katika duka hilo kwa Waziri wa Utalii, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Said Ali Mbarouk (kulia). Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Next Telecom, Zanzibar Bw. Mohamed Chanja.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Zanzibar Bw. Mohamed Mussa akiwa na Mkurugenzi wa Next Telecom, Zanzibar Bw. Mohamed Chanja mbele ya duka lililozinduliwa.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, imefungua duka jipya eneo la Muzamil, mtaa wa Mlandege hapa Zanzibar ikiwa na lengo la kuwarahishia wateja wake huduma pamoja na kuongeza wigo wa huduma kwa wateja.
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, imefungua duka jipya eneo la Muzamil, mtaa wa Mlandege hapa Zanzibar ikiwa na lengo la kuwarahishia wateja wake huduma pamoja na kuongeza wigo wa huduma kwa wateja.
Ufunguzi wa duka hilo unaenda sambamba na uboreshaji huduma wa kampuni ya Zantel pamoja na kuwezesha wateja wake kupata huduma kama simu, muda wa maongezi, modem pamoja na kadi za simu.
Duka hilo, lililo chini ya Next Telecom, pia litawawezesha wateja wa Zantel kutoa na kuweka pesa zao kupitia huduma ya EzyPesa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, ambao pia ulihudhuriwa na meneja wa Mauzo wa Emirates na Precision Air, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel hapa Zanzibar, Mohamed Mussa, alitoa shukrani za pekee kwa wateja wa mtandao huo kwa kuendelea kutumia huduma zao.
“Kampuni yetu imejikita katika kuhakikisha huduma zetu zinamfikia kila mtu hapa Zanzibar. Hivyo tuna uhakika duka hili litarahisisha sana huduma kwa wakazi wa Mlandege’ alisema Mussa.
Ufunguzi wa duka hilo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Utalii, Utamaduni na Michezo hapa Zanzibar, Mheshimiwa Said Ali Mbarouk ambaye aliipongeza Zantel kwa kuwa kampuni kubwa hapa Zanzibar lakini pia kwa kushinda tuzo ya mlipa kodi bora.
“Duka hili linaashiria namna kampuni ya Zantel ilivyo makini katika kuwapa wateja wake huduma bora na kwa urahisi. Huduma bora kwa wateja ndio msingi mkubwa wa ukuaji wa biashara’ alisema Mheshimiwa Mbarouk.
Mheshimiwa Mbarouk pia aliwaasa Zantel waendelee kutoa huduma bora kwa Wazanzibari huku pia akisisitiza ufunguzi wa maduka mengine ya aina hiyo ili kuwarahishia watuamiaji wengi wa simu.
Duka hilo jipya litakalokuwa likifanya kazi Jumatatu hadi Jumamosi, kuanzia saa tatu hadi saa kumi na moja jioni, linatarajiwa kupunguza msongamano kwenye maduka mengine ya Zantel yaliyopo Darajani, Mfereji wa Wima, Mchangani and Kokoni.