Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania,Sunil Colaso akiongea na meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja wao na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akimpa maelekezo ya huduma ya Airtel Yatosha mmoja wa wateja wa Airtel alietambulika kwa jina la Juliana wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja wao na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Afisa Mauzo wa Airtel bi Theresia Kimaro Akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel yatosha wakati Airtel walioko Magomeni na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali ikiwemo ya Airtle yatosha.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso Akibandika moja ya kipeperushi cha Airtel yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
---
Uzinduzi wa huduma Yatosha wafanyika rasmi Mwanza , Kanda ya
ziwa waanza kupiga simu kwa gharama nafuu Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kusambaza huduma ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini baada ya kuzindua huduma mpya ya punguzo la upigaji simu maarufu kama Airtel YATOSHA katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Airtel sasa imeanza kuitambulisha huduma hiyo kwa wadau na wateja wake katika mikoa mbalimbali nchini ili waweze kunufaika nayo Huduma ya Airtel Yatosha inamuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.
Akionge wakati wa utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wadau wa Airtel jijini Mwanza, Meneja wa kampuni hiyo kanda ya ziwa Ally Maswanya alisema" Tumeamua kushusha gharama hizo kutokana na maagizo ya mamlaka ya mawasiliano ambayo iliagiza gharama za simu kushushwa kutoka shilingi 112 kwa dakika hadi shilingi 34.92.
Kwa sasa huduma ya airtel yatosha ina punguzo la hadi asilimia 88 na inalenga kurahisisha mawasiliano kwa wateja wa hali zote kwa kuwawezesha kutumia kiwango kidogo cha fedha kupata muda wa maongezi wa kuanzia dakika 10 kupiga mitandao yote ,meseji bila kikomo na huduma ya internet".