Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Msanii Wema Sepetu amenusuru msanii mwenzake Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 na kumfanya awe huru katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na mumewe.
Mapema leo, Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya shilingi milioni 13, huku ikiwa ni kesi ambayo tayari ilishakuwa ngumu kwa mwanadada huyo.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na tuhuma za kutakatisha fedha haramu.
Faraji yeye amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213, huku mke wake akinusurika zaidi baada ya kutofaini yake na Wema Sepetu.
Kwa sasa Kajala yupo nyumbani kwao maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ndugu na jamaa.