Tigo Tanzania imetangaza kuwa Mdhamini mkuu wa Tuzo za wanawake Wenye Mafanikio Tanzania mwaka 2013 maarufu kama ‘Tanzania Women of Achievement Awards (TWAA) 2013’. Tuzo za TWAA hutolewa kila mwaka kutambua na kuenzi juhudi mbalimbali zinazofanywa na wanawake wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kuleta chachu ya mabadiliko na mtazamo chanya wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika maisha yao wenyewe na jamii zinazowazunguka.
Sherehe za kwatunuku wanawake walioleta chachu na mtazamo chanya katuika kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo zitafanyika mwezi Machi 28 mwaka 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar-es-salaam.
Wadhamini wengine wa Tuzo za TWAA mwaka huu ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Multi Choice Tanzania , Dar es Salaam Serena Hotel, East Africa Television, Cost Tech Consulting , Desktop Productions Tanzania (DTP), Zara Tours Tanzania, Africa Lynx Investment LTD, Deloitte na Frontline Porter Novelli.
"Tuzo za Wanawake wenye mafaniko Tanzania (TWAA) zilianzishwa mwaka kwa mara ya kwanza nchini 2009 kwa nia ya kuwatunuku wanawake wanaofanya kazi katika sekta mbalimbali nchini ambao kazi zao zimesaidia kuijenga jamii ya Kitanzania inayomzunguka kwa namna moja ama nyingine. Tunayo furaha kuwa tumepokea washindani wengi sana wenye vigezo vya kupta tuzo hizo, na tunasubiri kwa shauku kubwa kuwatunuku wale waliofanya vizuri zaidi siku ya sherehe. Tunawashukuru sana Wadhamini wetu, kwani bila wao tusingeweza kufanikisha zoezi hili. Tunatambua mchango wao mkubwa katika kuwawezesha wanawake, ambao ni kundi muhimu sana katika kulikusukuma mbele gurudumu la maendelo ya taifa. “ alisema Irene Kiwia, rais wa TWAA.
Bw. William Mpinga, Meneja Chapa wa Tigo alisema, "Tigo inatambua mchango mkubwa unaofanywa na wanawake wa Tanzania katika kulisukuma taifa hili lisonge mbele kimaendeleo na ninaona fahari kushirikishwa katika tukio hili la kipekee na la kujivunia linalolenga kuwazawadia wanawake ambao kupitia shughuli zao wameweza kufanikiwa na kutimiza malengo yao na kuweza kujitolea kuzisaidia jamii zinazowazunguka. Jamii zetu kwa sasa zinawahitaji sana wanawake wa aina hiyo ambao mafaniko yao yamekuwa ya thamani kubwa sana, siyo tu kwa wake na waume, bali pia kwa vijana wetu wa sasa”
Mpinga aliendela kufafanua kuwa, wanwake ni sehemu muhimu nay a thamani sana kwa jamii na kuuenzi mchango wao kutawaongezea ai na moyo wa kujituma zaidi katika kazi nzuri wazifanyazo kwa kuona kuwa zinatambuliwa.
Kamati TWAA mwaka huu 2013 inajumuisha, Bi Mary Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Tanzania Programu ya Mtandao wa Jinsia, Jaji Joaquine De Mello - Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga-aliyekuwa mwalimu wa taaluma, Chuo Kikuu cha Biashara Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo - Mtaalamu wa Jinsia-USAID, Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mtaalamu wa Ushauri wa Kisaikolojia na Sayansi ya Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Frontline Porter Novelli.