Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa (kulia) Kwanza ningependa kuwapongeza akinamama hawa kutoka Nepal kwa ujasiri waliouonyesha kwa kupanda mlima Kilimanjaro, na pia hilo lisingewezekana bila msaada wa Bodi ya Utalii ya Nepal hivyo tunawakaribisha sana Tanzania na tuko tayari kutangaza utalii baina ya nchi zetu hizi.
Leo tunasherehekea mafanikio ya kundi la akinadada kutoka Nepal ambao wamepanda mlima Everist lakini ili kuonyesha kwamba wanawake wakiwezeshwa wanaweza pia wamekuja kupanda Mlima Kilimanjaro. Tukio hili kwa ujumla litasaidia sana kuitangaza Tanzania katika Nyanja ya utalii ikizingatiwa kuwa waandishi kadhaa wa habari kutoka nje walikuwepo nasi tunaahidi kutoa ushirikiano.(Picha na Zainul Mzige Mo Blog)
Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Utalii ya Nepal Subash Niroula akizungumza na waaandishi wa habari ambapo amesema ukweli mafanikio ya program yatatufikisha mbali katika suala zima la utalii, ikizingatia hata sisi kuna vitu na vivutio vingi vya utalii vilivyopo Tanzania tulikuwa hatuvijui hivyo naamini tutafika mbali na kufanikiwa kuvutia watalii wengi zaidi. Kwa kweli tumepata fursa nzuri kuzungumza na idara ya utalii ya Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vya kipekee miongoni mwa nchi za Kusini Mwa jangwa la sahara.
Kwa nafasi hii pia watu watapata kuifahamu Nepal, kiutalii, kiutamaduni na zaidi ya hapo kupitia ushirikiano wetu na Tanzania.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumzia shirika lake lilivyoona umuhimu wa Program hiyo na kuamua kushiriki katika kuifanikisha.
Mratibu wa Msafara wa 7 Summit Women Team Shailee Basnet kutoka Nepal akielezea uzoefu wake baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro na Milima mingine ikiwemo milima Evarest ambapo wamekutana na mengi yakufurahisha na kuwashukuru Watanzania waliowapokea vizuri na kuwapa ushirikiano kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho.