Penzi Jipya ni kama Mkataba mpya wa kazi.... Penzi jipya ni tamu, linakufanya ujisikie raha kama mtu aliyepewa mkataba mnono wa ajira baada ya kutafuta kazi kwa msoto kwa muda mrefu. Unapata mshawasha na kimuhemuhe huku mapigo yako ya mdukuo wa moyo yakiwa juu ukidhani hali ile itakuwa hivyo milele lakini sivyo.
Kabla hujaingia uhusiano mpya punguza munkari. Usiwe na pupa, soma mazingira kwanza ili ujue kama utaweza kuhimili dhoruba za humo ndani.
Umejiandaaje ukikuta Bosi wako, New partner, ni kimeo?... Kabla hujasaini mkataba wa kazi, hata uwe mnono namna gani usome vizuri ili ujue kama vitu vyote muhimu unavyohitaji kwenye mkataba vimeandikwa. Dont be in a rush!
Wengi husaini mikataba ya Relationship kwa pupa kwasababu they are in need au kuangalia hela tu, mwisho wa siku unakuta Mkataba haukupi Health Insurance unaanza kujuta kwanini ulisaini... Sijui kama mmenielewa!
Imeletwa kwenu na Seth Giovanni,
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mapenzi.