Chumvi inapotumika kwa kiasi kidogo haina madhara. Miili yetu huhitaji chumvi kwa kiasi kidogo sana. Kwa wastani tunahitaji chini ya gramu 5 (kijiko cha chai) kwa siku.
Hii huupatia mwili madini ya sodium yanayohitajika kwa siku. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba mwili unapata pia madini haya kutoka kwenye vyakula vingine, hivyo chumvi itrumikeitumike kwa kiasi kidogo.
Hii huupatia mwili madini ya sodium yanayohitajika kwa siku. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba mwili unapata pia madini haya kutoka kwenye vyakula vingine, hivyo chumvi itrumikeitumike kwa kiasi kidogo.
Kwa bahati mbaya tunatumia chumvi kupita kiasi, matumizi ya chumvi nyingi yanaongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu, kwani chumvi nyingi husababisha maji kujikusanya mwilini.
Maji yaliyo jikusanya huongeza shinikizo kwenye moyo na mishipa ya damu na hivyo husababisha moyo kufanya kazi kwa nguvu zaidi.
Shinikizo kubwa la huongeza uwezekano wa kupata magonjwa mengine sugu kama yale ya figo, moyo na pia ya mifupa kama “osteoporosis”.
Shinikizo kubwa la huongeza uwezekano wa kupata magonjwa mengine sugu kama yale ya figo, moyo na pia ya mifupa kama “osteoporosis”.
Hivi karibuni tafiti zimeonyesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya vyakula vilivyosindikwa au kuhifadhiwa kwa chumvi na saratani ya tumbo.
Hivyo ni muhimu kupunguza saratani ya chumvi.
Je nifanye nini ili niweze kupunguza matumizi ya chumvi?
- Kupunguza matumizi ya chumvi kutasaidia kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa sugu. Yafuatayo yatasaidia kufikia lengo hilo:
- Punguza chumvi inayowekwa kwenye chakula wakati wa kupika.
- Usiongeze chumvi kwenye chakula wakati wa kula, pia usiweke chumvi mezani, mara nyingi watu huongeza chumvi bila hata kuonja chakula.
- Epuka vyakulavilivyosindikwa kwa kutumia au kuongeza chumvi, kama nguru aliyekaushwa kwa chumvi, baadhi ya vyakula vya kopo paketi.(kama supu za paketi au makopo “soy source” michanganyiko ya kunogesha mchuzi, crips). Ni vyema kusoma lebo kwa makini na chagua vyakula vilivyoandikwa “hakuna chumvi iliyoongezwa” (no salt added)
- Tumia zaidi vyakula fresh unavyopika mwenyewe kwani unaweza kuthiubiti kiasi cha chumvi unachotumia.
- Tumia zaidi zaidi viungo kuongeza ladha kwenye chakula, mfano vitunguu saumu, tangawizi n.k.
Kama umezoea kutumia chumvi nyingi inaweza kuchukua muda kidogo kujizoesha kula chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi. Jizoeshe taratibu mpaka uzoee na mwisho utafurahia vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi.