Mary Chrisostom Rutta, kutoka Mkoa wa Manyara (katikati) akifurahi baada ya kutangazwa mshindi. Kushoto ni Jamia Abdul (Kagera) na Joan John kutoka Lindi ambao waliingia tatu bora.
Ilikuwa ni shangwe na furaha tupu kwa washiriki na ubunifu wao.
Mwakilishi wa Kagera, Jamia Abdul, akicheza ngoma ya Kihaya.
MREMBO Mary Rutta kutoka Mkoa wa Manyara jana usiku aliwabwaga warembo wenzake 26 katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Miss Utalii mwenye kipaji. Kinyang’anyiro hicho kilifanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)