Wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakigonganisha glasi za mvinyo wa matunda ya Mananasi uliotengenezwa nchini Burundi wakati wa hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kwenye maonyesho ya utalii ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin jijini Berlin Ujerumani, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na mkakati wa Kutangaza utalii wa Afrika Mashariki na mwaka huu ilikuwa na kazi moja ya kunadi maajabu manne ya Afrika yaliyopatikana katika ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mto Nile, Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro Crater huku Tanzania ikiwa kinara kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa maajabu yake matatu ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na Ngorongoro Crater jambo lililofanya itamkwe mara nyingi miongoni mwa viongozi waliopata nafasi kuzungumzia utalii wa Afrika Mashariki. PICHA NA FULLSHANGWEBLOG Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akipokea tuzo maalum iliyotolewa na iliyotolewa kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Bi Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye maonyesho ya (ITB) Berlin jana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC) Jesica Eriyo. Bi. Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hotuba yake na kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utalii wa nchi za Afrika MasharikiNaibuKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Bi Jesica Eriyo akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo ili azungumze na washiriki wa maonyesho hayo pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo.Ken Nyauncho Osinde Balozi wa Kenya nchini Ujerumani akizungmza na wageni waalikwa na kueleza ushirikiano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani katika kutangaza utalii wa ukanda huoKatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Tanzania Bi Maimuna Tarishi akitambulishwa rasmi katika hafla hiyoMaofisa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kulia ni Bw. MashauriBrenda Mugambi na Aileen Mallya wakiwa katika hafla hiyo.KaimuBalozi wa Tanzania nchini Ujerumani Chrisopher Mvula kushoto akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki katika hafla hiyo. Makatibu wakuu na Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi na maofisa wa Utalii wa Nchi za jumuiya ya Afrika MasharikiMakatibu wakuu na Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi na maofisa wa Utalii wa Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
↧