Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

AFYA YAKO: FAHAMU MAFUTA BORA KWA YANAYOFAA KATIKA CHAKULA

$
0
0
Je mafuta yapi yaliyobora kutumia?
Mafuta ni muhimu mwilini, isipokuwa yanahitajika kwa kiasi kidogo; hivyo kuepuka kabisa ulaji wa mafuta huweza kuleta athari katika mwili, ikiwemo ubongo kutofanya kazi vizuri. Hata hivyo mafuta yanapotumika kwa kiasi kikubwa yanaweza kuleta madhara mwilini. Hivyo ni muhimu kuwa makini na kiasi cha mafuta kinacholiwa katika kila mlo.
Kuna aina kuu mbili za mafuta; yale yanayopatikana katika vyakula vya asili ya wanyama nay ale yatokanayo na mimea.
  1. Mafuta yenye asili ya wanyama
Mafuta yenye asili ya wanyama huwa yameganda katika joto la kawaida. Mafuta haya ni kama nyama iliyonona, nyama ya nundu, samli, siagi, jibini na maziwa yenye mafuta.
Mafuta haya hayana lehemu kwa kiasi kikubwa. Utumiaji wa mafuta haya huongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kuwa na uzito uliozidi na unene uliokithiri au kisukari. Hivyo ni muhimu kupunguza utumiaji wa mafuta haya.
  1. Mafuta yatokanayo na mimea.
Mafuta yatokanayo na mimea huwa katika hali ya kimiminika katika joto la kawaida na kwa kawaida haya hayana lehemu. Mafuta haya ni kama mafuta ya soya, ufuta, karanga, alizeti, mawese, pamba na nazi.
Mifano mingine ni pamoja na mbegu zitoazo mafuta kama korosho, kweme na mbegu za maboga. Mafuta haya ndio bora zaidi kuyatumia ukilinganisha na yale yenye asili ya wanyama kwani huboresha afya ya mwili. Hata hivyo ni muhimu kuyatumia kwa kiasi kidogo.
Mara nyingi nimesikia lehemu ni mbaya, je ina ubaya gani?
Lehemu inahitajika mwilini lakini kwa kiasi kidogo. Hata hivyo huwezi kujua una lehemu kiasi gani mwilini mpk upime (kwa kawaida inatakiwa iwe chini ya 200mg/dl). Kiasi kikubwa cha lahemu mwilini husababisha mkusanyiko wa mafuta katika mishipa ya damu na hivyo huweza kuzuia damu kupita kwa urahisi.
Hali hii huweza kusababisha shinikizo kubwa la damu na ugonjwa wa moyo. Hatari nyingine ni mafuta kuziba mishipa midogo ya damu inayoenda kwenye moyo au ubongo na hivyo kusababisha kiharusi na hata kifo.

Waweza kupunguza hatari hii kwa:
  • Kupunguza utumiaji wa nyama, mayai, jibini, na maziwa yasiotolewa mafuta, maini, firigisi, figo. Unapotumia nyama nyekundu isizidi nusu kilo kwa wiki.
  • Kuepuka mafuta yatokanayo na wanyama, nyama zilizo nona, ngozi ya siagi na mafuta
  • Kuongeza matumizi ya vyakula yenye makapi-mlo kwa wingi kama nafaka zisizokobolewa mfano unga wa dona, ulezi, uwele, mtama vyakula vya jamii ya kunde, mboga mboga na matunda. Kwa kawaida vyakula vyenye makapi-mlo kwa wingi havina mafuta mengi.
  • Kufanya mazoezi ya mwili angalau dk 30 kila siku.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles