
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akikabidhi vifaa vya ngoma za asili kwa Ismail Edward Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam hivi karibuni, huo ni msaada aliouahidi kwa shule hiyo baada ya kuonekana kuna uhaba wa vifaa vya muziki wa asili shuleni hapo, wanaoshuhudia tukio la makabidhiano hayo katika picha katikati ni walimu Venance Njiku na Bi. Nickyza Bwenge, vifaa hivyo ndivyo vilivyotumiwa na kikundi cha ngoma za asili cha shule hiyo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo yakishirikisha wazazi, wageni waalikwa mbalimbali , Bodi ya shule pamoja na uongozi wa wanafunzi wa shule hiyo.




