KUJITUMA ni msingi wa mafanikio na kuthamini kile ulichonacho kama unavipaji zaidi ya kimoja jiwekee mikakati thabiti ya kuweza kuvitumia vyote kwa pamoja ili kuweza kufanikisha malengo yako uliojiwekea hayo ni maneno ambayo anayatumia prodyuza wa Surround Sound studio Emanuel Maungu anajulikana kwa jina la Ema Theboy katika msingi wa kuyaongoza maisha yake.
Mbali na kutengeneza muziki taaluma yake ni mwalimu, ambapo alianza mafunzo hayo ya ualimu mwaka 2010-2012 daraja la tatu A huku akiwa amepangiwa mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kufundisha,ingawa kwa kipindi hicho chote anafanya kazi ya kutengeneza muziki
Baada ya kumaliza masomo yake ya O level ndipo alipopata nafasi ya kujiunga na chuo cha ualimu mkoani Tanga, ambapo aliweza kufanikiwa kusoma kwa kipindi cha miaka mitatu, na kuweza kuhudhuria masomo kwa vitendo na kukumbwa na changamoto kadhaa kama mwalimu, huku akiweka wazi kuwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika ni moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wawapo katika mazingira ya kazi hiyo
Alianza kupenda muziki tangu akiwa mwanafunzi ambapo alijiunga na kwaya kanisani ili aweze kupata nafasi ya kujifunza kutumia baadhi ya vyombo vya muziki ikiwemo Kinanda, ingawa aliweza kufundishwa 'key' moja ya herufi A, kutokana na juhudi zake binafsi aliweze kumudu kujifunza key nyingine ambapo mpaka sasa ndio muongozo wa kazi zake.
Ema the Boy akiwa mshiriki wa BSS 2013 |
Kutokana na hali ya kupenda kutengeneza muziki alijikuta akilazimika kujiunga na Nyumba ya kukuza Vipaji (THT) mwaka 2012 ambapo alianza kujifunza kutumia 'Technology' mpya ya kuhamisha muziki kwenye kinanda na kutumia computa kutengeneza muziki
Kutokana na ugumu wa technology alikaa wiki moja bila ya kuingia studio ili aweze kujipanga na kujifunza huku akipata darasa la walimu kuhusu matumizi ya technoilogy hizo mpya ambazo kwake zilikuwa ngeni
Hali hiyo iliweza kumsaidia na kumudu kutengeneza muziki i wenye hadhi ya kimataifa na kujitofautisha na maprodyuza wanaofanya muziki wa kuchora
Kazi yake ya kwanza kama Prodyuza ilikuwa ni kutengeneza nyimbo ya 'Upepo' iliyoimbwa na msanii Recho wa kutoka kundi la THT alichukua wiki nzima kuikamilisha wimbo huyo huku akiwa amesimamiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kupata muongozo na kuboresha nyimbo hiyo
Kwa kuwa ni nyimbo yake ya kwanza na alikuwa anaamini kile anachokifanya, hivyo aliamini kuwa nyimbo hiyo ingeweza kufanya vizuri na ndivyo ilivyokuwa kwani nyimbo hiyo ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri katika 'gemu' la muziki nchini
Prodyuza huyo hakuishia hapo aliamua kujiwekea mikakati iliyothabiti ili aweze kuboresha kazi zake kwani ameweza kuendelea kutengeneza muziki wenye radha tofauti huku akiamini kuwa hawezi kusikiliza muziki alioutengeneza kila wakati ili kuepusha kurudia rudia nyimbo zinazofanana
"Napenda kuwa mbunifu kwenye kazi zangu naepuka sana kurudia kazi hivyo nina mikakati iliyo thabiti ili kuendelea kuboresha kazi zangu ziweze kuwa nzuri n zenye kuvutia"
Ili kuonyesha kuwa anaendelea kuifuata mikakati yake ya kutengeneza muziki yenye ubora na kujitofautisha na maprodyuza wengine ameweza kutengeneza nyimbo nyingine zinazofanya vizuri kwenye 'gemu' la muziki 'Me and U' ya msanii Ommy Dimpoz, pamoja na nyimbo ya Barnaba inayojulikana kwa jina la 'Sorry'
Siku za mapumziko anapenda kuangalia katuni na movi, huku rangi anayoipenda zaidi ni blue na nyeusi
Ameweka wazi kuwa anamchumba anayempenda huku akisisitiza mwanamke anayempenda ni yule anayeelewa kitu anachofanya na kuthamini pamoja na kuheshimu yake anayoyafanya