Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

BARAZA LA MICHEZO TAIFA NA BRITISH COUNCIL YAFANYA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA MAOFISA HABARI MJINI MOROGORO

$
0
0
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Maria Mbora Nkya akifungua Semina ya waandishi wa habari za michezo na Maofisa mbalimbali hapa nchini juzi katika Semina Mjini Morogoro. Pembeni yake ni Mratibu waSemina hiyo kutoka Baraza la MIchezo Taifa (BMT)Jacob Nduye.
Mwezeshaji wa Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi na Maofisa bi. Leanne Martin-Pollock akifafanua jambo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini.
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania Mwani Nyangassa akifafanua jambo kwa Maofisa wa habari, Kulia ni Sakina Mfinanga na Adrophina Ndyeikiza.
Mkufunzi wa Semina hiyo Sauda Simba akifafanua jambo.
Mwandishi mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo ASha Kigundula akitoa ufafanuzi juu ya utendaji kazi wa vyombo vya habari.
Baadhi ya Maofisa wakifanya kazi za makundi.
Mhariri wa Gazeti la Nipashe Amour Hassan akifafanua jambo juu ya utayarishaji wa Gazeti lao.
Afisa habari wa Mwanza, Bw. Kuni akifafanua jambo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Maria Mbora Nkya amewataka waandishi wa habari za michezo nchini kujiepusha na habari za uchochezi ambazo zinaweza kuleta sintofahamu kwa jamii husika na kusababisha vijana kutojikita katika michezo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku nne mjini Morogoro kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa huo Elia Mtanda alisema, wanahabari endapo wataepukana na habari hizo wataisaidia kuelimisha jamii kwa ujumla.
“Wanahabari nyie ni watu muhimu sana katika jamiii na ndio maana wanaomba sana kuepukana na habari za uchochezi katika michezo, ambazo zinaweza kushusha kiwango cha michezo hapa nchini,”alisema.

Aidha Nkya alisema, lengo kubwa la semina hii ni kuwapa elimu wanahabari ili waweze kuifanyia kazi na kuwaelimisha watu wengi katika jamii kutokana na umuhimu wa michezo hapa nchini.
Alisema, anaimani Semina hii itawasaidia wanahabari kuwaelimisha vijana kuipenda michezo mbalimbali na kupata ajira ikiwa ni kujiajili wao wenyewe bila ya kuwa tegemezi.
“Mafunzo haya yawe chachu kwenu na kuwafanya vijana kupenda michezo ili kujiajili na kuepuka kuwa tegemeo kwa kuwa michezo ni ajila tosha kwa vijana wetu hapa nchini,” alibainisha.

Semina hii imeandaliwa na Baraza la michezo Taifa (BMT), kwa kushirikiana na British Council inatarajia kufikia tamati Machi Mosi mwaka huu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>