Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

AFYA YAKO: TOFAUTI YA JUISI HALISI NA JUISI BANDIA

$
0
0
Je kuna tofauti gani kati ya juisi halisi ya matunda na juisi bandia?
Juisi halisi ya matunda ni juisi ambayo inatokana na kukamuliwa matunda, mara nyingi bila kuongeza maji au sukari, japo ipo aina ya matunda ambayo inakuwa bora ukiongeza maji kidogo kama vile pesheni, maembe, mananasi nk. Juisi halisi za matunda zilizotengenezwa kiwandani huandikwa “100% juice” na mara nyingi huwa bei ya juu.
Juisi bandia ni pamoja na vinywaji vyenye rangi mbali mbali vinavyouzwa madukani, ambavyo ni mchanganyiko wa maji,sukari, rangi na ladha bandia ya matunda.
Vinywaji hivi hata kisheria haviruhusiwi kuitwa juisi. Vinapokuwa ndani ya pakiti au chupa kwenye lebo huongezwa neon “Drink” na hivyo kusomeka “Juice-drink”. Hii ina maana sio juisi halisi ya matunda.
Nyingine zimewekwa juisi kwa kiasi kidogo tu kwa hiyo ukisoma lebo utaona asilimia ya juisi iliyowekwa.
Vinywaji hivi bandia kwa kiasi kikubwa huchangia kuupa mwili nishati-lishe nyingi na havina virutubishi vingine, hivyo huchangia ongezeko la uzito, pia huhusishwa na kuongezeka uwezekano wa kupata saratani za aina mbali mbali.
 Sio kweli kwamba vinywaji hivi vinapokuwa na rangi ya zambarau au nyekundu huongeza damu, bali vinywaji hivyo vimeongezwa rangi ambayo haina virutubishi vyovyote.

Je unashauriwa kula mayai mangapi kwa siku?
Mayai yana protini kwa wingi, pia vitamin na madini. Hata hivyo mayai yana lehemu kwa wingi. Yai moja lina kiasi cha miligramu 213 ya lehemu, ambacho ni kiasi cha lehemu kinachohitajika mwilini kwa siku.
Hivyo ni bora kupunguza matumizi ya mayai, yasizidi matatatu kwa wiki na litumike yai moja tu kwa siku tofauti.
Kumbuka vyakula vingine pia vina lehemu na vile vile mwili hutengeneza lehemu.

Je, kati ya maziwa fresh na mtindi yapi ni bora zaidi?
Maziwa fresh au mtindi yana virutubishi muhimu hasa protini, madini na vitamin unaweza kutumia maziwa aina yoyote kutegemeana na matumikzi yake.
Hata hivyo maziwa ya mtindi huyeyushwa kwa urahisi zaidi tumboni na pia husaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine na ufyonzwaji wa baadhi ya virutubishi, Hivyo maziwa ya mtindi yanapendekezwa zaidi hasa kwa wagonjwa kwani yanamsaidia mgonjwa kupata virutubisho vingi zaidi kwa haraka. Maziwa ya mtindi pia yana aina ya bacteria wazuri ambao huweza kuzuia au kutibu fangasi katika mfumo wa chakula.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>