Afisa Rasilimali watu wa Airtel Bi Doris Kibasa akikabithi vitabu kwa mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo mchango uliotolewa na wafanyakazi kwa watoto wa shule yenye mahitaji maalumu. wafanyakazi wa Airtel walitoa mchango huo walipotembelea shule ya msasani Jana.
Afisa Rasilimali watu wa Airtel bi Monica Mbwilo vitabu kwa mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo mchango uliotolewa na wafanyakazi kwa watoto wa shule yenye mahitaji maalumu. Wafanyakazi wa Airtel walitoa mchango huo walipotembelea shule ya msasani Jana
Msimamizi wa miradi kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Mubaraka Kibarabara akimkabithi mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo vitabu vya wanafunzi na vya walimu ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanywa na wafanyakazi wa Airtel katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu.
Watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya msasani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononiya Airtel mara baada ya kupokea msaada wa vitabu kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo vilivyotolewa kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa Airtel ili kusaidia ufundishaji wa masomo ya elimu kwa watoto wa mahitaji maalumu shuleni hapo
---
wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkoni Airtel kwa pamoja wameshiriki katika kuchanga na kusaidia wanafunzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalumu iliyopo Msasani jijini Dar es salam.
Wafanyakazi hao wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 3 zilizotumika kununua vifaa mbali mbali vya kufundishia.
Akizungumzia mpango huo maalum wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Afisa Rasilimali watu wa Airtel Bi Doris Kibasa alisema “mkakati huu umewahusisha wafanyakazi wa Airtel katika vitengo tofauti, ninawashukuru kwa kujipanga wao wenyewe na kutumia muda wao kwa kuwakumbuka watoto hawa kwa namna hii
Zoezi hili limewezesha upatikanaji wa jumla ya vitabu vyenye thamani shilingi milion 3 kwa shule ya msasani na kupunguza uhaba wa vitabu kutoka kitabu kimoja kwa watoto watatu hadi kitabu kimoja kwa kila mtoto mmoja.
“tumeona mahitaji ya wanafunzi hawa tulipotembelea shule hii mwishoni mwa mwaka jana. Na kuamua kujipanga ili kuweza kuwasaidi wadogo wetu na majirani zetu ili waweze kufika hapa tulipo sisi leo. Tunaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumeweza kuinua maisha ya watoto hawa na kiwango cha Elimu hapa Tanzania” alisisitiza Bi Doris
nae Mwalimu Mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum Bw, Lessy Nyambo alisema msaada huo ni mkombozi kwa wanafunzi hao kwani utawawezesha wanafunzi hao kuwa na kitabu kimoja kimoja badala yakutumia kitabu kimoja wanafunzi wawili mpaka watatu. Amesema kwamba wanafunzi hao wanakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi vitakavyowawezesha kuendelea na masomo bila tatizo lolote na hivyo amewahasa mashirika ya umma na wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu
Nae mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Msasani Fatuma Ally aliishukuru Airtel kwa kuweza kuwapatia Vitabu ambavyo vitaweza kuwasaidia katika masomo yako.
Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imedhamiria kuendelea kuboresh kiwango cha elimu nchi na kuleta mabadiliko katika masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi wasayansi nchini.
Wiki mbili zilizopita tumetoa msaada wa Vitabu na sare za shule katika shule ya msingi ya Kiromo iliyopo mjini Bagamoyo vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 , huku ikitoa msaada wa vitabu kwa shule 4 za sekondari kwa kila mkoa ikiwemo mikoa ya Kagera na Mwanza Lengo ni kufikia shule nyingi zaidi nchini Nzima.