WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamanolililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya
kujadili changamoto wanazozipata wadau hao.
kujadili changamoto wanazozipata wadau hao.
waziri wa ajira na kazi Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau waliouthuria katika konga mano hilo.
Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Bg Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni mkurugenzi wa VSO Tanzania.
Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Bg Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni mkurugenzi wa VSO Tanzania.
waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji mwenyekiti wa bodi. |
Waziri kabaka wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi ayupo pichani kuhusiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(Veta).
Baadhi ya waandishi wakiendelea kufatilia kwa makini kongamano hilo.
Washiriki wakifuatilia.
Picha wakwanza kulia ni mwenyekiti wa bodi ya veta Idrissa Mshoro wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi wakiwa wanamsikiliza waziri (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akiwa anaongea katika kongamano hilo
wadau kutoka sekta ya gesi na petrol wakiwa wanafatilia.
katibu mkuu wa VET Pro.Sifuni Mchome akiwa anawakilisha mada.
Na Woinde Shizza, Arusha
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo hivi sasa.
Hayo yanesemwa leo jijini hapa na WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana
Aidha aliwataka vijana kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze kujiariri badala ya kufanya biashara za kuuza vitu mikononi bali watumie taaluma walizozipata kuzalisha vitu vyenye ubora.
Alisema vijana wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya uhakika.