Ndege ya Fastjet FJA FN141 inayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza, ikiwa imebeba abiria 142 iliruka kutoka airport ya kimataifa ya Julius Nyerere mida ya takribani saa 12:49 asubuhi siku ya Alhamisi ya tarehe 4 Disemba 2014.Muda mfupi baada ya ndege kuruka chombo hicho kilikumbana na ndege aliyekuwa akiruka. Kama sehemu ya maangalizi rubani wa ndege hiyo aliamua kugeuza safari na kurudi katika uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Ndege ilitua salama bila kashikashi zozote zile. Abiria wote na wahudumu wa ndege walikuwa salama bila majeruhi ya aina yeyote ile.Abiria waliwekwa kwenye ndege za baadae na mida ya safari za Fastjet za siku hiyo zilibadilika kimasaa kutokana na msukosuko huo. Injini ya ndege husika ilirekebishwa ndani ya siku moja na kuendelea na shughuli zake kesho yake siku ya tarehe 5 Ijumaa Disemba 2014.
Uongozi wa Fastjet unasisitiza kuwa usalama ni kitu muhimu zaidi kwa kampuni ya Fastjet na inashukuru kwa uelewa wa wateja wote na kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.