Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Sanato Mhenge (kushoto) akipokea mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia Nchi kutoka kwa mwenyekiti wa bodi wa Forum CC Euster Kibona ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Naibu wake Ummy Ali Mwalimu wakimsikiliza meneja mwezeshaji wa Taasisi ya Forum CC Rebeca Muna wakati wakipokea mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia Nchi unaoendelea kufanyika Lima nchini Peru.
Ujumbe wa Forum CC ukiongozwa na meneja mwezeshaji wake Rebeca Muna (kushoto), katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Binilith Mahenge(wapili kutoka kushoto) na Naibu Waziri wake Ummy Mwalimu(katikati), pamoja na mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster Kibona (wa pili kutoka kulia) na ofisa maendeleo wa Forum CC Adam Anthony. wakati wa makabidhiano ya mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano mkuu wa kimataifa wa TabiaNchi.
Akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya waziri mwenye dhamana na Mazingira Mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema serikali inapaswa kubainisha mapendekezo ya kupunguza makali ya uharibifu wa mazingira kwa nchi zilizoendelea. Pia nchi zilizoendelea zikubali kuwepo na makubaliano ya kisheria na kuheshimu kanuni juu ya masuala yote ya mazingira.
Kibona ametoa wito kwa viongozi wa dunia na Afrika kuwashirikisha wadau wengine katika mchakato wa mikataba ya kimataifa ili kupunguza manung’uniko ya kutoshirikishwa kwa wadau. Pia amesema nchi zilizoendelea zinapaswa kutoa fedha ,teknolojia na kujenga uwezo juu ya kukabiliana na janga la uharibifu wa mazingira.