Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka(mwenye tai nyekundu), akimsikiliza Muongozaji Ndege katika kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Bi. Mossy Kitang’ita, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), leo asubuhi katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka hiyo.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC), Bw. Nyello S. Abeid, akimueleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambapo maonesho hayo yameanza leo tarehe 3 na yataendelea mpaka tarehe 5/12/2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Kaimu Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa katika Usafiri wa Anga na Maji kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambayo yanafanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akimsikiliza Mhandisi Kutoka Wakala wa Ndege za Serikali(TGFA), Mhandisi Trophese Mwambo wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho yanayofanyika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo asubuhi. Maonesho hayo yamelenga kutoa elimu kwa umma juu ya maswala mbalimbali yanayohusu Usafiri wa Anga Tanzania, wakati Sekta ya Usafiri wa anga ikitimiza miaka 70 ya ushirikiano na wadau mbalimbali duniani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Ofisa Utawala, kutoka Baraza la Ushauri la Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA-CC), Ms Catherine Monarya, wakati alipotembelea banda hilo kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo, Katibu Mkuu ameishauri taasisi hiyo kutoa elimu zaidi ya haki za watumiaji wa Usafiri wa Anga kwa wananchi.
Wadau mbalimbali wakipata maelezo ya vifaa mbalimbali vinavyotumika katika Viwanja vya Ndege Nchini Tanzania kutoka kwa mtaalam wa Mamlaka ya VIwanja vya Ndege Tanzania(TAA),Thomas Protas, walipotembelea katika banda hilo kufahamu maswala mbalimbali yanayohusu usafiri wa Anga. Maonesho ya ya Usafiri wa Anga yanafanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka hiyo kuanzia tarehe 3 mpaka 5 Desemba 2014.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere(JNIA), Bw. Malaki Moses, akimuelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo, katika maonesho ya Usafiri wa Anga. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mamlaka ya USafiri wa Anga Tanzania(TCAA).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka akimsikiliza, Afisa Mawasiliano na Masoko wa shirika la Ndege la Fastjet, Bi. Lucy Mbogoro, wakati alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Usafiri wa Anga yanayofanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, akisisitiza jambo wakati alipotembelea banda la Swissport, leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya ya Usafiri wa Anga Tanzania. Wa kwanza kulia ni Meneja Masoko wa Shirika hilo, Bw. James Mhagama. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakati wakisherekea miaka 70 ya Usafiri wa Anga.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)