Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19576

SYDS KWA KUSHIRIKIANA NA MAREKANI KUWAKOMBOA WAKULIMA PAWAGA IRINGA

$
0
0
Mwakilishi wa ubalozi wa marekani David Feldmann akihutubia mamia ya wakazi wa vijiji vya tarafa ya Pawaga (hawapo pichani) wilayani Iringa mkoa wa Iringa wakati sherehe ya kufunga mafunzo ya mradi wa kuwawezesha  wanachama  wa  vikundi 43 vyenye wanachama 300 katika kilimo kupitia asasi ya mpango salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) chini ya ufadhili wa watu   wa marekani (Picha  na MatukiodaimaBlog).
Wasanii   wakionyesha  igizo jinsi  watakavyonufaika na asasi hiyo.
Mwakilishi wa balozi wa Marekani David Feldmann wa  pili  kulia akifuatilia  burudani mbali mbali
Baadhi ya  viongozi  wakimsikiliza mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini
Wanakikundi  wakiwa katika mkutano  huo wakimsikiliza mwakilishi  wa balozi
Baadhi ya  wana  kikundi  watakaonufaika na taasisi  hiyo
Wananchi  Pawaga  wakifuatilia  mkutano huo
Wanahabari  Iringa  wakimhoji  mwakilishi wa balozi  wa Marekani Nchini Bw David Feldmann
Msanii kutoka mjini Iringa  akionyesha  ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya  chatu kwa kujaribu  kumumeza 

TAASISI  isiyo ya  kiserikali ya mpango  wa maendeleo salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) chini ya ufadhili wa ubalozi wa marekani  nchini Tanzania  ikmekusudia kuwainua kwa  kilimo wanachama wa vikundi 43 katika tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa  vijijini mkoani Iringa 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati sherehe ya kufunga mradi huo wa mrejesho kwa vikundi, meneja mahusiano wa SYDS, Arnold Pangani alisema SYDS imejitoa  kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto zinazowakabili wengi wa akina mama katika sekta kilimo nchini.

Pia  alisema hadi  sasa  tayari  wamekwisha  toa mafunzo ya kilimo  bora kwa  wanachama  zaidi ya  300 katika tarafa  hiyo.

“SDYS kwa udhamini wa serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania tunaungana kwa pamoja na wananchi wa Pawaga zaidi tukitambua ushiriki wa wanawake katika kilimo,” alisema Panagani.

Aidhi, wanavikundi walitoa shukrani ya dhati kwa SDYS kwa kuwapatia mwongozo bora ambao umewawezesha kupata uelewa juu ya elimu ya mpango biashara na uendashaji vikundi.

Walisema kuwa kuja kwa asasi ya SDYS kumeweza kuhamasika na kuunda vikundi ambavyo vitasaidia katika shughulu za kilimo.

Walisema kwa mafunzo hayo kama vijana wametambua umuhimu wao kama vijana ni nguvu kazi na wanatakiwa kushiriki  shughuli za maendeleo na kujifunza zaidi juu ya mpango salama kwa maendeleo ya vijana.

Kwa upande wake mwakilishi wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania, David S. Feldmann alisema Tanzania itajengwa na watazania wenyewe na marekani itajengwa na wamarekani.

Alisema kuwa matatizo ya watanzania hayawezi kumalizwa na marekani isipokuwa katika uwezekaji ndiyo suluhisho matatizo yote.

Alisema ni jukumu kwa kila mwananchi kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika kuinua na kukuza uchumi.

Alisema watanzania lazima walipe kodi kwa serikali iliwaweze kupatiwa huduma stahiki kutoa kwa serikali kama ilivyo marekani.

Alisema kuwa asilimia 90 ya serikali ya marekani inaendeshwa kwa mapato ya ndani kwa vile wananchi wengi wanalipa kodi kwa serikali bila kutegemea misaada ya nje.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19576

Trending Articles