Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki
Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Muhitimu aliyefanya vizuri Shahada ya Kwanza ya Jinsia na Maendeleo, Nyamambara Simon katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika Dar es Salaam leo. W apili kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila.
Vyeti vikiendelea kutolewa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa- Kutoka kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph na Mjumbe wa Bodi Dk.Terezya Huvisa (MB).
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (wa pili kushoto), naye alikuwepo na waalikwa wengine.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu hao wakiwa kwenye sherehe hizo.
Mwanahabari, Msuya Selemani (katikati), akiwa na wanafunzi wenzake baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Siasa na Uendeshaji wa Maendeleo ya Jamii.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mwanahabari, Msuya Selemani akiwa katika mahafali hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph, akizungumza katika mahafali hayo.
Ndugu wa wahitimu hao wakifuatilia matukio mbalimbali katika mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mjumbe wa Bodi ya Chuo, Dk.Terezya Huvisa MB (kushoto), akitoa shukurani kabla ya kuhitimisha mahafali hayo.
Wahitimu hawa wakitafakari jambo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
Blasi band ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwaaga wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na viongozi wa chuo hicho.Na Mwandishi Wetu.
SERIKALI imeendelea kufanya jitihada za dhati kwa ajili ya kukabiliana na kushuka kwa ufaulu katika vyuo mbalimbali nchini.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angela Kairuki wakati akihutubia katika mahafali ya tisa ya katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Alisema juhudi hizo za Serikali ni pamoja na Mpango wa Elimu ya Shule za Misingi, Mpango wa Elimu ya Sekondari, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi wa miaka Mitano 2013-2014 na 2017-2018 na Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)
"Jitihada hizi zinaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini.
Kairuki alisema juhudi za Serikali zimeanza kuzaa matunda na kujionesha kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu katika shule za Sekondari nchini.
Aliongeza kuwa bajeti finyu ya chuo hicho ni changamoto ambayo ipo katika vyuo mbalimbali vinavyo milikiwa na serikali nchini na kuwa lengo la Serikali ya awamu ya nne ni kuimarisha vyuo vya elimu ya juu ili viweze kutoa elimu iliyobora.
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila alisema changamoto kubwa ya chuo hicho ni pamoja na tatizo la uhaba wa hosteli katika chuo hicho cha Kivukoni na Tawi la chuo hicho Zanzibar hivyo kuwafanya wanafunzi kuishi uraiani.
Alisema katika Kampasi ya Kivukoni, chuo kinahosteli tatu zenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzio 480.
"Katika mwaka wa masomo wa 2013/2014 wanafunzi walioishi kwenye hosteli za chuo nio wanaume 214 na wanawake 266" alisema Mwakalila.
Aliongeza kuwa katika mwaka wa masomo wa 2013/2014 jumla ya wanafunzi 998 sawa na asilimia 67.57 ya wanafunzi 1478 waliishi nje ya chuo na kuwa idadi zaidi ya wanafunzi wanaoishi nje ya chuo inategemewa kuongeza mwaka hadi mwaka.
Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 689 walitunikiwa cheti, Stashahada ya Kawaida na Shahada ya Kwanza ambapo wanawake ni 400 sawa na asilimia 58.1 na wanaume ni 289 sawa na asilimia 41.9.
Mwaka huu kuna upungufu wa wahitimu 231 sawa na asilimia 25.03 ukilinganisha na mwaka jana ambapo walikuwa 919.