Lonjino ni mwajiriwa katika kampuni moja ya usambazaji wa nyama.
Siku moja jioni baada ya kumaliza kazi zake za siku aliamua aingie katika chumba baridi cha kuhifadhia nyama kukagua kitu na kwa bahati mbaya mlango ukajifunga huku akiwa ndani.
Alijaribu kugonga mlango na hata kupiga kelele za kuomba msaada kwa muda mrefu lakini jitihada zake hazikufanya lolote kwani kutokana na barafu zilizomo ndani na jinsi kulivyozibwa kuzuia ubaridi kutotoka nje haikuwa rahisi kilio chake cha kuomba msaada kusikika.
Haikuwa rahisi kusikika sauti yake kutoka katika chumba hicho na kila mfanyakazi alikuwa ameshaondoka.
Masaa manne baadae Lonjino alikuwa kama yuko katika bonde la umauti akisubiri kifo chake huku akimwomba Mungu wake kwa sala yenye unyenyekevu mkubwa.
Akiwa katikati ya sala yake mara akashtushwa kuona mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na mlinzi wa kampuni hiyo akiingia na kumwokoa.
Wakiwa katika chumba kingine huku Lonjino akiwa kapewa msaada wa moto ili kuupasha mwili wake joto na kahawa ikiwa Mezani, Lonjino akaamua amuulize yule mlinzi ni kitu gani kilimfanya akifungue chumba kile.
Mlinzi akamjibu, "Nimefanya kazi katika kampuni hii kwa miaka 21 na katika kipindi hiki mamia ya wafanyakazi wamekuwa wakiniona kama mtu nisiye na maana na ni wachache sana wanaonisalimia kwa kuniambia HABARI ZA ASUBUHI wakiwa wanaingia kazini na KAZI NJEMA wanapoondoka jioni kurudi makwao.
Leo asuhuhi ulipoingia ulinisalimia kwa furaha kama kawaida yako na jioni wakati watu wanaondoka kurudi kwao nikaisubiri sauti yako kunifariji tena kwa kusema KAZI NJEMA kama siku nyingine lakini sikuisikia ndio nikaamua kuanza kupitia kila chumba kuona nini kimekupata na ndio nikakuona kwenye chumba kile ukiwa umefungiwa"
Funzo:
Tuishi maisha ya kupendana na kuwajali wale watuzungukao kwani huwezi jua ni namna gani kwa kufanya hivyo tunawapa furaha katika maisha yao na kuwafariji.