Maelekezo Muhimu.
- Wahitimu wa kidato cha sita mwaka2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo,Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita,Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbijiwamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
- Wahitimu hawa waliochaguliwawanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoakama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wakuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.
- Zoezi la usajili litaanzashuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanziatarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
- Atakaeamua kuripoti kwa Kamandawa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shuleya Polisi Tanzania mjini Moshi.
- Vijana hawa watalazimika kufikashuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
- Vyeti vyao vyote vya masomo (original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birthcertificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
- Mashuka mawili rangi ya BluuBahari (light blue)
- Chandarua chenye upana futitatu
- Nguo za michezo(Track suitnyeusi,Tshirt blue na Raba)
- Pasi ya Mkaa Ndoo moja
- Pesa za kulipia bima ya afyakiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).
- Pesa kidogo ya kujikimu.
- Kwa mujibu wa kanuni za shuleya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikanana simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanyamawasiliano.
- Angalia orodha kwenye tovuti yawww.policeforce.go.tz au fikaOfisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara yamahakama kuu.