Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MKE WA JAJI JOHN RUHANGISA ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GARI, ARUSHA

$
0
0

 Mke wa Jaji John Ruhangisa, Marehemu Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa enzi za uhai wake.

 Jaji John Ruhangisa.
 Jaji John Ruhangisa (wa pili kushoto), akiwa na watoto wake wakati wa ibada ya mazishi ya mke wake Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa iliyofanyika nyumbani kwake katika Kijiji cha Ibwera mkoani Kagera leo jioni. Kutoka kulia ni mtoto wake wa kwanza Moreen, David na Fiona.
 Mapadre 30 wa Kanisa Katoliki wakiwa kwenye ibada hiyo ya mazishi.


 Viongozi mbalimbali , majaji, watawa na wananchi wakiwa kwenye ibada hiyo.


 Watawa wakiwa kwenye ibada hiyo.




 Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Ibwera nao walikuwepo kutoa burudani.
 Watoto wa Kanisa Katoliki wanaoshiriki kuongoza ibada mbalimbali wakiwa kwenye ibada ibada hiyo.


 Watoto wa Kijiji cha Ibwera nao walijumuika katika mazishi ya mama yao Kokuhengesa.
 Jaji John Ruhangisa akimfariji mtoto wake David.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Bukoba, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Hery Mwaibambe akimpa pole  mtoto wa marehemu, David.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa wakielekea kaburini tayari kwa mazishi.

Jaji John Ruhangisa akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya mke wake.
 Padre aliongoza ibada hiyo akiweka msalaba katika kaburi la Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa.
 Jaji John Ruhangisa akifarijiana na watoto wake Moreen (kulia) na Fiona. Hakika inahuzunisha.
 Jaji John Ruhangisa na watoto wake wakiweka shada la maua kaburini.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr. James Rugemalira akisaini katika  kitabu cha maombelezo.
 Mdau Erick Kashasha naye alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliosaini katika kitabu cha maombolezo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akisaini katika kitabu cha maombolezo.

Dotto Mwaibale

SIMANZI na majonzi viligubika leo jioni  katika mazishi ya mke wa Jaji John Ruhangisa, Marehemu Laetitia Kokuhangisa Ruhangisa aliyefariki kwa ajali ya gari jijini Arusha.

Mazishi hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Ibwera katika mkoani Bukoba.

Viongozi  mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa, Majaji, dini na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya mkoa wa Bukoba walikuwa ni miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi hayo.

Akizungumza katika mazishi hayo Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Dk. Emmanuel Ugirashebuja alisema kifo cha mke wa Jaji Ruhangisa kiliwashitua na kuwahunisha.

"Kifo cha mke wa mwenzetu kimetusikitisha sana kwani marehemu enzi za uhai wake tulikuwa tukijumuika naye kwa mambo mbalimbali kwa kweli tupepoteza mtu muhimu" alisema.

Ugirashebuja alisema mafanikio yote aliyoanyo Jaji John Ruhangisa yametokana na maisha ya upendo aliyokuwa mke wake kwake ndio maana alipata fursa ya kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa hakuwa na matatizo nyumbani kwake.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na majaji kadhaa akiwemo Rais aliyepita wa  Mahakama ya Afrika Mashariki, Jaji Nsekela, Jaji Rutakangwa aliye mwakilisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Mwakilishi kutoka Halmshauri ya Meru.

Mke wa Jaji Ruhangisa alipoteza maisha Oktoba 29 mwaka huu  Tengeru mkoani Arusha wakati akitoka kazini baada ya Hiace aliyokuwa amepanda kugongwa na lori la mafuta.

Katika ajali hiyo watu 12 walipoteza maisha wakiwemo maofisa elimu watatu wa Halmshauri ya Meru.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles