Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kufanya mkutano na viongozi wakuu dini nchini lengo likiwa ni kujadili njia ambazo zitaweza kusaidia nchi kupambana na ujangili nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu amesema kwamba mkutano huo utakuwa na mafanikio makubwa kwani anaimani viongozi hao wataweza kushawishi umma kwa hali na mali kuweza kupamabana na suala zima la ujangili wa wanyama nchini.
Aidha Waziri Nyalandu amesema kwamba bado anahitaji mbinu zaidi za kupamaba na suala hilo hivyo amealika nchi tisa kuweza kushiriki majadiliano yapomaoja ya kikanda kwa jinsi ya kupamaba na biashara haramu ya madawa ya kulevya na ujangili.
Hivi karibuni waziri huyo alizindua rasmi mkakati wa taifa wa kuapamba na ujangili dhidi ya tembo na biashara haramu ya pembe za ndovu.