Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), wakisubiri kujua hatima ya maombi yao ya kuongezewa mishahara yao kutoka sh.240,000 wanazolipwa hadi kufikia sh.500,000 kama walivyokubaliana na serikali katika mkutano uliofanyika katika Karakana ya TRL Dar es Salaam jana. Wafanyakazi hao wameanza mgomo kushinikiza kulipwa kiasi hicho cha mshahara baada ya serikali kudaiwa kushindwa kutekeleza maombi yao.
Wafanyakazi hao wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wafanyakazi hao wakiuchapa usingizi wakati wakisubiri majibu yao.
Treni la abiria likiwa limeegeshwa Kituo cha stesheni Dar es Salaam jana. Haikuweza kufahamika kama lilikuwa likiendelea na safari zake baada ya mgomo huo au la.