Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Kiislamu, Sheikh Said Mwaipopo (katikati) akiwa na Katibu Baraza la Habari la Kiislamu, Chief Msopa (kushoto) pamoja Kiongozi wa Islamic Peace Sadiki GodiGodi wamewaasha wamewaasa waislamu kupinga maandano yaliyopangwa kufanyika leo tar. 14.2.2013 na kesho tar. 15.2.2013 baada ya swala ya Ijumaa wakati Sheikh Ponda Issa Ponda akipelekwa mahakama.
Maandamano yameandaliwa na Kondo Juma Bungo wakishirikiana na taasisi ya Shura ya Maimamu, yamelenga kuanzia tarehe 14,15 mahakamani, kwa ajili ya kutaka kumtoa Sheikh Ponda Isa Ponda.
"Tunachosema sisi kama sehemu ya waislamu ikiwa baraza la habari la Kiislamu tunawaomba waislamu wote wawe wastamilivu na subira kwa sababu nchi ya Tanzania si nchi ya kijeshi wala mabavu bali ni nchi ya kisheria na kanuni".
Tunawataka wale vingozi walioasisi maandamano hayo waweze kufuata taratibu za kisheri, kwa sababu kama watafanya maandamano wataonyesha moja kwa moja kwamba wao wanataka kuongeza tatizo na si kupunguza tatizo.
Walisema kuwa Sheikh Ponda alikamatwa kwa kisheria na taratibu za nchi ya Tanzania na wanaomba aachiwe kwa mujibu wa kisheria na taratibu za nchi, waliongeza kuwa kukamatwa kwa Ponda, waumini wote wanaumia kwa vile ni kiongozi wao, sheikh wao katika imani na kitanzania lakini taratibu wanazotaka kufuata hazikidhi matakwa ya nchi ya Tanzania maana hazionyeshi utu na uungwana katika taifa.
Kwa utafiki walioufanya wamegundua kwamba maandamano hayo hayana maslahi yeyote na uislamu ila yanamaslahi na kikundi cha watu binafsi na vile vile yanamaslahi na kundi la wanasiasa lililopo nyuma yao, hivyo wanawataka waislamu wawe makini maana si kila anayetangaza maandamano ana nia nzuri na uislamu.
"Kuna watu wanatangaza maandamano kuwa ni waislamu kumbe si waislamu lengo lao si uislamu na kama lengo ni uislamu wangeshirikishwa masheikh wote, taasisi zote za dini ya kiislamu wakakaa kwa utaratibu wakafatilia taratibu za dhamana kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi basi sheikh Ponda angedhaminiwa".
Lakini kuonyesha wazi watu hao hawashida na uislamu wala hawana nia ya kumtoa Ponda bali wanania ya kuleta vurugu maana wamekaa kikundi cha watu wachache pale Uwanja vya Mwembe Yanga wakitoa maneno ya vitisho kwa waumini na viongozi wa dini ya kiislamu kuwa watawakata vichwa na kuwamwangua tindikali.
"Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi Tanzania liwaangalie kwa makini watu hao ambao wanataka kuvunja amani ya nchi ya Tanzania kwani yaliyotokea Zanzibar yasije yakatokea tena hapa Tanzania bara yasitokea.
Kiongozi wa Islamic Peace Foundation, Sheikh Sadiki GodiGodi akitilia msisitizo.