Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala yake kwenye hafla hiyo ambapo alitoa pongezi kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Umoja huo kuhakikisha malengo ya milenia yanafikiwa kwa asilimia mia moja.r.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati hafla hiyo ikiendelea.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Tibaijuka kuzungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Profesa Tibaijuka na Bw. Rodriguez wakijiandaa kufanya "cheers" ya kuutakia kheri Umoja huo.
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakigonganisha glass "Cheers" kuutakia kheri Umoja huo kwa kutimiza miaka 69.
Pichani juu na chini baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo mabalozi na wadau wa taasisi mbalimba za serikali na zisizoza kiserikali waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar mwishoni mwa juma.
Kwa picha zaidi ingia humu