Mhariri wa Gazeti ya Citizen la hapa nchini,Bw. Richard Mbamba ambaye ni mmoja kati wanahabari waliowahi kushinda tuzo za "CNN MultiChoice African Journalist of the Year 2008" akisisitiza jambo wakati wa Semina ya simu moja kwa wanahabari wa Tanzania juu ya namna wanavyopaswa kufanya kazi zao,iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika,jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imekuja ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika wa shughuli ya utoaji tuzo hizo za "CNN MultiChoice African Journalist of the Year 2014" itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
Sehemu ya wanahabari waliohudhulia Semina hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa toka kwa baadhi ya wanahabari nguli barani Afrika walioongoza semina hiyo.
Mhariri wa Gazeti ya Citizen la hapa nchini, Bw. Richard Mbamba akiendelea kutoa somo kwa wanahabari.
Mhariri wa Gazeti la City Press la nchini Afrika Kusini, Ferial Haffajee akizungumza wakati wa Semina ya simu moja kwa wanahabari wa Tanzania juu ya namna wanavyopaswa kufanya kazi zao,iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika,jijini Dar es Salaam.
Mwandishi akifafanua jambo.
Baadhi ya Wanahabari wa Tanzania wakiuliza maswali kwa wahariri hao.
Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam
Ushauri umetolewa kwa waandishi wa habari nchi kuongeza juhudi na maarifa katika kazi zao ili kuweza kupata tuzo bora za kimataifa.
Akizungumza katika semina iliyoandaliwa na kituo cha CNN cnn katika suala zima la kuwani Tuzo za African Journalist Award Mahariri wa Gazeti la The Citizen nchini Richard Mgamba amesema kwamba ipo haja kwa Tanzania nayo kuweza kushiriki na kushinda kwani hakuna jambo lililotofauti na nchi nchi nyingine ambalo Tanzania halipo bali ni nia na ubora wa kazi pekee.
Akizungumzia semina hiyo Mwandishi wa Gazeti la Daily Newz nchini Anna Rhobby alisema kwamba semina hii imeweza kuwapa moyo na kujijua kuwa nao kama waaandishi wa Tanzania wanaouwezo wa kushiriki na kushinda kwani hakuna kitu tofauti katika story za hapa nchini na za nje ya nchi.
Mashindano hayo yanatarajia kufanyika siku ya jmosi wiki hii kwa mwaka huu yanafanyika hapa nchini na ni mshiriki mmoja kati ya washiriki 1600 kutoka bara la Afrika ametoka Tanzania ambapo ameingia katika final.