Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akisalimiana na Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) kabla ya kuanza kwa matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana yaliyodhaminiwa na kampuni hiyo. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya saratani ya Ocean Road, Diwani Msemwa (kushoto kwake) na Mkurugenzi wa Wellworth Tanzania, Saul Basckin.
Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akiongea na watu waliohudhuria matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya saratani ya matiti Kunduchi Beach Hotel jana.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (wa tatu kushoto) akiongoza matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana yaliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo. Kulia ni Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya saratani ya Ocean Road, Diwani Msemwa (kushoto kwa waziri)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akifanya mazoezi kabla ya kuanza matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana, Matembezi hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo.
Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akizungumza machache.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ,Dk. Seif Rashid akiongea na watu waliohudhuria matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya saratani ya matiti Kunduchi Beach Hotel jana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Simu za mkononi Tigo wakipozi kwenye picha ya pamoja baada ya matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana.
Shoo love mara baada ya matembezi.
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii dkt Seif suleiman Rashid amefanya matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi na matibabu ya saratani ya matiti lengo likiwa ni kuchangisha fedha takriban million 130 ili kutokomeza saratani hiyo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza matembezi hayo Dkt Rashid amesema kwamba zaidi ya watu elfu 44 wa hapa nchini kila mwaka hugundulika na ugonjwa wa saratani ya matiti ambapo asilimia 80 ya ya wagonjwa hao hufika hospitalin wakiwa na hali mbaya hali ambayo haina matibabu.
Naye corporate Responsibility Manager wa kampuni ya simu ya mkononi Tigo Woinde Shisael amesema kwamba wao kama tigo wanapenda kuwahamasishwa wanawake kuweza kufanya uchunguzi mapema ili wapate matibabu ya haraka na wapone kwani ugonjwa huo unatibika.
Kampuni ya Tigo ni moja ya wadhamini wa matembezi hayo ambapo zaidi ya wafanyakazi 300 wa Kampuni hiyo wameshiriki katika matembezi hayo yaliyo anzia hortel ya kunduchi beach hadi njiapanda.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “KWA MOYO NA MATARAJIO TUNAWEZA KUWA NA TANZANIA HURU ISIYO NA SARATANI YA MATITI”