Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya kasi ya 3G katika mnara wa Tigo mpakani Namanga, mkoani Arusha. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini David Charles na Mwenyekiti wa Kijiji cha Namanga Mheshimiwa William Kikois (kushoto).
Mhandisi wa Kanda wa Kaskazini kutoka Tigo Judika Anosisye (kulia) akimuonyesha kifaa cha dish ya 3G (hakipo pichani) kilichofungwa juu ya mnara a Tigo iliyopo mpakani Namanga, wilayani Longido, mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (Kushoto) akijaribu kutumia intanet ya Tigo baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kasi ya intanet ya 3G katika mnara wa Tigo iliyopo Namanga, wilayani Longida, Arusha. Kulia ni Mhandisi wa Kanda wa Kaskazini kutoka Tigo Judika Anosisye akiendelea kutoa maelekezo kuhusu kifaa hicho kipya cha 3G kinachoonekana kwenye picha, huku Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini David Charles (kati kati) akishuhudia.
Mnara wa Tigo yenye uwezo wa kasi wa intanet ya 3G kama unavyoonekana eneo la Namanga.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya akizungumza na baadhi ya wananchi wa Namanga wakati wa ufunguzi wa mnara huo juzi wilayani Longido.