Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki
Katika picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja.
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi katika hafla hiyo, kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
Muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.