Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

AIRTEL YAZINDUA MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI VYA MUZIKI KUPITIA SIMU YA MKONONI YAJULIKANAYO KAMA AIRTEL TRACE MUSIC STAR

$
0
0
Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star" kwa lengo la kukuza na kuvumbua vipaji vya wana muziki chipukizi na kuwawezesha kufikia ndoto zao. Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon, uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam.


Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akiongea wakati wa Uzinduzi wa program ya Airtel Trace Music Star , program itakayowawezesha wanamuziki chipukizi kuonyesha vipaji vyao vya muziki kwa kupitia simu zao za mkononi.






Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimples akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star"kwa lengo la kukuza na kuvumbua vipaji vya wana muziki chipukizi na kuwawezesha kufikia ndoto zao. Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon. uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akifatilia kwa karibu uzinduzi wa program ya kusaka vipaji vya muziki ijulikanayo kama Airtel Trace Music Star.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiwa na msaani wa muziki wa kizazi kipya Lady JD wakati wa uzinduzi wa Airtel Trace Music Star.

Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi Kipya AY (pili kulia) akijadiliana jambo na mtayarishaji wa muziki nchini,Lamar wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star Program inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon. uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam.wengine pichani ni Mtangazaji maarufu nchini Salama Jabiri pamoja na Blogger Shamim Mwasha.
MC Ephrahim Kibonde akiongoza hafla hiyo.
Wadau wa burudani.
Mazungumzo ya hapa na pale.

Wadau hawa pia walikuwepo kwenye hafla hiyo.
sehemu maalum ya vilaji kwa walaji.
Wanalibeneke wakijadiliana mambo,toka kushoto ni Faustin,Kajuna na Othman.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mashindano ya
kusaka vipaji vya muziki kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama
Airtel TRACE Music Star kwa lengo la kukuza vipaji vya muziki na
kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa kitanzania kujulikana katika anga
za muziki duniani

Uzinduzi huu umefatia ushirikiano kati ya Airtel na Kampuni Muziki ya
TRACE pamoja na mwanamuziki nguli wa Marekani Akon

Mashindano haya mbali na kufanyika nchini Tanzania pia yatashirikisha
vijana kutoka nchi 13 barani Afrika ambazo Airtel inafanya biashara
zake, nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi,
Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic
Republic of Congo (DRC), na Gabon, ambapo waimbaji bora kutoka kwenye
kila nchi watachaguliwa na kuzawadiwa baada ya kuingizwa kwenye
mashindano yatakayowashirikisha waimbaji bora kutoka nchi nyingine ili
kupata mshindi atakayetwaa taji la Mwanamuziki mwenye kipaji bora
Afrika. Mshindi wa Afrika atajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo
kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni
pamoja na kufaidika na mafunzo ya kufuliwa kimuziki na Nguli wa Muziki
wa Amerika Akon.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa program hiyo Mkurugenzi wa Masoko bwana
Levi Nyakundi alisema” mpango huu unaenda sambamba na dhamira yetu wa
kuwawezesha vijana wenye ndoto ya kuwa wanamuziki bora kuonyesha uwezo
wao kuwawezesha kufikia ndoto zao. Tunafahamu kuwa Tanzania ina vijana
wengi wenye vipaji vya muziki lakini bado hawajajulikana katika anga
za muziki na ndio maana leo tunazindua program hii na kuwawezesha
kujiunga kirahisi kupitia simu yake ya mkononi na kushirikia Airtel
Trace Music Stars na kuibuka kuwa wanamziki bora”.

Mashindano haya yatakayoenda kwa muda wa mienzi sita yanaanza kuanzia
rasmi hapa nchini siku octoba 7 2014 ambapo mshiriki yeyote
atakayependa kushiriki atatakiwa kupiga 0901002233, na kuimba nyimbo
zake kwa kutumia simu yake na kutuma kwenye namba hii, kisha nyimbo
zake zitasikilizwa na kuchagulia kufudhu kuingia kwenye kinyanganyiro
na kuweza kupigiwa kura kuibuka kuwa mwimbaji nyota wa Tanzania na
baadae kuwa super star wa Afrika kwa ujumla.

Halikadhalika mashabiki na wapenzi wa muziki wataweza kumpigia kura
mshiriki wanayempenda ili kumuwezeshwa nyimbo zake kushinda, ili
kumpigia kura mshiriki wako tuma namba/code ambayo mshiriki
ataitangaza pindi nyimbo yake itakapochaguliwa kuingia kwenye
mashindano au unaweza kuipata wewe mwenyewe kwenye tovuti
www.tracemusicstar.com’’Aliongeza Nyakundi.

Akiongea kuhusu program hiyo Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimpoz alisema’ kwa hakika haya ni mashindano ya pekee yanayotoa fulsa kwa mwanamziki yeyote ambaye angependa kuwa superstar kushiriki.

Napenda kuwahamasisha vijana kuchangamkia fulsa hii kwa kurekodi
freestyle yako ya flave yoyote kali kupitia simu yako na kutuma
nyimbo yako. Pia napenda kuwaomba mashabiki na wapenzi wa muziki
kuwapigia kura washiriki hawa kwa wingi ili kuweza kumpata ushindi.
kwa wanamuziki chipukizi mashindano haya si yakukosa maana wewe pia
unaweza kuibuka kuwa superstar wa Airtel Trace Music Star kwa njia
rahisi tu Piga, Imba, Shinda. aliongeza Dimples.

Airtel imeingia mkataba wa ushirikiano na Trace Music kwa muda wa
miaka mitatu ambapo Fainali ya mashindano haya ya Airtel Trace Music
2014 yanategemea kufanyika Mwezi March 2015.


Zawadi nyingine zitakazotoliwa kwa washindi wa mashindano haya ni
pamoja na pesa taslimu na simu za mkononi

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles