Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior akitizama maadhari ya jiji la Mwanza baada ya kuwasili leo mchana kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika leo Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza.
100 usikose Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza.
WAFANYABIASHARA wanao miliki vituo vya radio, television pamoja na kumbi za burudani nchini wameaswa kuwekeza katika muziki wa reggae kwa kuanzisha vituo maalum vya kupiga muziki huo na kumbi maalum za muziki huo kwani ni sekta ambayo ni fursa iliyo wazi kwa kuwa soko lake lipo si kwa vijana tu bali hata kwa watu wazima.
Hayo yamesemwa na Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior ambaye yuko jijini Mwanza katika ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa barani Afrika akitoa burudani ya muziki huo na kuutambulisha uzuri wake kwa jamii kizazi na kizazi ambapo kesho (Ijumaa) kwa mara ya kwanza atakutana na mashabiki wake pale Villa Park kwenye Tamasha lake linalojulikana kama REGGAE BRING BACK LOVE.
Dj Steve Junior anasema kuwa ni kwa takribani miaka kumi sasa amewekeza katika muziki huo akiburudisha na kuufanya muziki huo kuwa sehemu ya kuendesha maisha yake, familia na jamii yake.
Dj Steve Junior anasema kuwa ni kwa takribani miaka kumi sasa amewekeza katika muziki huo akiburudisha na kuufanya muziki huo kuwa sehemu ya kuendesha maisha yake, familia na jamii yake.