Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Ushauri umetolewa kwa serikali kuweza kutoa elimu kwa wananchi pindi katiba itakayopendekezwa itakapo kabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete ili wawe na uelewa mpana katika kupiga kura za maoni kuhusiana na katiba hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa majadiliano yaliyohusu rasimu iliyotolewa hivi karibuni bungeni, Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi amesema lengo la kongamano hilo ni kuwajengea wananchi kuelewa vizuri masuala ya katiba ili kuweza kupata katiba iliyobora na yenye kuzingatia jinsia.
Aidha LIUNDI amesema kwamba ipo haja wanawake wote kupigania suala zima la 50 kwa 50 liingie katika katiba mpya ili ifikapo mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu wananwake nao wawe kipaumbele kugombea nafasi mbalimbali.
Naye mjumbe wa mtando huo, Usu Mallya amewasihi wanawake kuhakikisha masuala yote ya wanawake na jinsia yanaingia katika agenda muhimu pamoja nakuhakikisha yanaendelea kufanyiwa kazi siku zote.