Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MKALI WA BONGO FLAVA DIAMOND PLATNUMZ WAKISHIRIKIANA NA MZIIKI

$
0
0
 Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki kama  Brand Partner. Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya wasanii pekee wa Afrika walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa mwakilishi wa bidhaa hiyo akiwakilisha nchi yake.

"Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwasasa ni Brand Partner wa Mziiki," anasema Arun Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa, watengenezaji wa Mziiki. 

"Kwa kushirikiana na msanii mwenye kiwango kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki. 

Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ilikuendelea kuhakikisha kwamba watumiaji wetu na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na kupanua wigo wa wateja wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia.

 Nadhani pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa muziki streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa kukumbuka hilo. "

Mziiki ni huduma pekee inayokupa Miziki ya kiafrika kupitia Streaming, huduma ambayo inatoa safu mbalimbali ya muziki kutoka Afrika na kimataifa. "Mimi nimepata mzuka kujiunga na Mziiki," anasema Diamond. "Programu na simu (mobi) tovuti ni nafasi kubwa kwa ajili ya wasanii kupanua idadi yao ya mashabiki na kutambulisha mara ya kwanza single yao mpya kusikika bara la Afrika na dunia."
Mziiki ni programu ya simu iliyoundwa kwa ajili ya Music Streaming iliyosheheni miziki ya Afrika. 

Imepata umaarufu haraka ikiwa na mkusanyiko mkubwa wa sauti safi na vipaji kipekee vinavyokidhi miziki ya kiafrika. Programu hii ni rahisi kutumia, inamakala ambayo huru husum tumiaji kushirikisha marafiki wimbo wa upendao au kuwatumia nyimbo kama miito ya simu ya nyimbo walizochagua. Makala haya yamewekwa kuwawezesha wasanii, kama Diamond, kufikia mashabiki wapya katika Afrika na dunia ni kote.

"Mziiki kweli imenipa zaidi ya kile ambacho ningeweza kuomba" Anasema Diamond. "Mimi situkuwapatia mashabiki wangu nafasi ya kupata nyimbo zangu zote bali pia pia kupata nafasi ya kupanua wigo wa mashabiki wangu kupitia programu ya“Share and Dedicate” . Wakati mashabiki wangu wakishirikisha au wakituma wimbo wangu wowote maalum kwa wenzao, nania juaye waweza kusambaa kwa kiasi gani?Mimi tayari nimeshaanza kuona idadi ya mashabiki wangu ikiongezeka kwa namna hii.

Ikiwa na kiwango kizuri na kuongezeka kwa orodha ya wasanii waliosajiliwa kutoka katika bara la Afrika, Mziiki ni mahali ambapo wasanii wapya wanaweza kwenda kuzindua kazi zao na wasanii waliopo sasa kuendelea kukua.

Mziiki ni program ya Mobile Streaming iliyoundwa ilikukidhi mahitaji ya msanii na mashabiki kwa jumla. Mziiki ilianzishwa mwezi Mei 2014, na imesaidia kuongeza mafanikio katika kazi za wasanii na inaendelea kukua kila siku na kuwa wezesha wasanii kufurahia zaidi kama ilivyo kwa Diamond Platnumz.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles