
Mashindano hayo yanashirikisha timu mkoa wa kipolizi wa Kinondoni ambazo zinatoka katika maeneo ya Kimara, Kawe, Tegeta, Mabibo na Ubungo wachezaji wakiwa ni waendesha Booda, awamu ya kwanza ya ligi hiyo ilikuwa na timu 32 na sasa ni awamu ya pili ambapo timu 16 zinashindana ili kupata timu 8 zitakazoshiriki Ligi ya Nane Bora na hatimaye kupata mshindi wa mashindano hayo ya Kinondoni Bodaboda Cup ambaye atapata zawadi nono.
Lengo la Mashindano hayo ni kuwakutanisha waendesha Bodaboda wote wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ili waweze kufahamiana wao kwa wao, lakini pia ili jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liweze kuwaelimisha juu ya sheria za usalama Barabarani na Ulinzi Shirikishi kwa jamii.





Kikosi cha timu ya Tegeta kikiwa katika picha ya pamoja kalba ya kuanza kwa mchezo huo timu hiyo imefungwa magoli 3-0 na timu ya Kawe.

Baadhi ya mashaifuatilia mchezo huo.


Kutoka kulia ni Aghata Isack Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Esther Ngaja Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Refarii wa mchezo huo Geofrey Mwamboneke, Mshika Kibendera Hamis Pondamali, Mshika Kibendera Mwanahamisi Matiku, ASP. Emilian Kamuhanda Insp.Soud Ramadhan na Mratibu wa kombe hilo Ernest Mbaga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers leo.
